Pata taarifa kuu

Ukraine: Ishirini na Saba wakubaliana juu ya msaada wa euro bilioni hamsini

Nchi 27 za Umoja wa Ulaya zimefikia makubaliano, Alhamisi, Februari 1, juu ya msaada wa euro bilioni hamsini kwa miaka minne kwa Ukraine, hadi wakati huo ukiwa umezuiwa na Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban. Hata hivyo  Viktor Orban amekaribisha uanzishwaji wa "utaratibu wa udhibiti" juu ya matumizi ya pesa ya Kyiv.

Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel na Rais wa Tume Ursula von der Leyen wakiwa na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky mnamo Februari 3 huko Kyiv.
Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel na Rais wa Tume Ursula von der Leyen wakiwa na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky mnamo Februari 3 huko Kyiv. AFP - HANDOUT
Matangazo ya kibiashara

 

Mashaka hatimaye yalidumu kwa muda mfupi wakati wa mkutano huu usio kuwa wa kawaida. Tangazo hilo linatoka kwa Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel: “Umoja. Viongozi wote 27 wamekubaliana juu ya msaada mwingine wa euro bilioni 50 kusaidia Ukraine ndani ya mfumo wa bajeti ya Umoja wa Ulaya. Mkataba huu unahakikisha ufadhili thabiti, unaotabirika na wa muda mrefu kwa Ukraine," afisa huyo ameandika kwenye X (zamani ikiitwa Twitter), mwanzoni mwa mkutano wa kilele usio kuwa wa kawaida huko Brussels, Alhamisi Februari 1, 2023.

Kutoka Kyiv, Ukraine imekaribisha "mchango" wa Umoja wa Ulaya kwa "ushindi wa pamoja" dhidi ya Urusi. "Ni muhimu sana kwa uamuzi ulichukuliwa na viongozi 27, ambao kwa mara nyingine tena unathibitisha umoja wenye nguvu wa Umoja wa Ulaya," Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekaribisha siku ya Alhamisi, baada ya kuondolewa kwa kura ya turufu ya Hungary kwenye mfuko huu. Msaada huu "utaimarisha utulivu wa muda mrefu wa kiuchumi na kifedha, ambao sio muhimu kuliko usaidizi wa kijeshi" kwa Kyiv dhidi ya uvamizi wa Urusi, ameongeza.

Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amekaribisha "siku njema kwa Ulaya" na Kyiv imekaribisha "mchango" wa Umoja wa Ulaya kwa "ushindi wa pamoja" dhidi ya Urusi.

Maelewano yaliyofikiwa yanatoa uwezekano wa kuitisha mkutano wa kilele wa wakuu wa nchi au serikali ndani ya miaka miwili kuchunguza utekelezaji wa bajeti hii ya kila mwaka ya Ulaya. Mkutano huo ulitanguliwa na mkutano ulioongozwa na Viktor Orban uliowaleta pamoja Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, mkuu wa serikali ya Italia Giorgia Meloni, pamoja na Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen na Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel. "Tunahitaji makubaliano ya nchi 27," amesisitiza Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz alipowasili.

"Ishara muhimu"

Misaada ya Ulaya iliyokusudiwa kwa Ukraine (mikopo yenye thamani ya euro bilioni 33 na michango yenye thamani ya euro bilioni 17) imejumuishwa katika nyongeza ya bajeti ya Umoja wa Ulaya hadi mwaka 2027. Msaada ambao Kiev inahitaji sana kuweka uchumi wake sawa, huku mfuko wa msaada wa Marekani ukizuiwa katika Bunge la Congress. "Hii ni ishara muhimu kwa Ukraine kwamba EU itasimama nyuma yenu kwa muda mrefu, hadi ushindi," amesema Waziri Mkuu wa Estonia, Kaja Kallas.

Kiongozi huyo wa Hungary, pekee kati ya wale Ishirini na Saba aliyedumisha uhusiano wa karibu na Moscow baada ya kuanzishwa kwa uvamizi wa Ukraine karibu miaka miwili iliyopita, aliamsha hasira za viongozi wenzake waliokusanyika mnamo mwezi Desemba mwa uliyopita kwa kupinga msaada huu wa kifedha. Alishutumiwa mjini Brussels kwa kuihujumu EU ili kupata kutolewa kwa fedha za Ulaya zilizokusudiwa kwa ajili ya nchi yake lakini alifungiwa kutokana na ukiukaji wa utawala wa sheria uliokosolewa huko Budapest.

Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban alihalalisha mabadiliko yake ya moyo kwa ukweli wa kupokea "dhamana" kwa mabilioni ya euro zilizotengwa kwa Budapest na kusimamishwa na Brussels. "Tuliogopa kwamba pesa zinazodaiwa na Hungary na ambazo kwa sasa zimehifadhiwa na Tume ya Ulaya zingeishia Ukraine," amesema kwenye video iliyowekwa kwenye akaunti yake ya Facebook. Hata hivyo "tulipokea dhamana" kwamba hii haitakuwa hivyo, ameongeza bila maelezo zaidi, pia akikaribisha kuanzishwa kwa "utaratibu wa udhibiti" juu ya matumizi ya fedha ya Kyiv.

Mkutano wa kilele katikati ya uhamasishaji thabiti

Waziri Mkuu wa Poland Donald Tusk amekariri ukosefu wa subira unaoongezeka alipowasili Brussels. "Hatujachoka na Ukraine, tumechoka na Viktor Orban," ametangaza, akishutumu "mchezo wa ajabu na wa ubinafsi" wa Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban.

Mkutano huo unafanyika katikati ya maandamano makubwa ya ulimwengu wa kilimo: matrekta 1,300 yalikusanyika katika tamasha la honi, hadi Brussels. Waandamanaji walikabiliana na polisi nje ya Bunge la Ulaya, ambapo matairi yalichomwa moto na sanamu kuangushwa, karibu na eneo la mkutano huo.

Wakati wa mkutano wa kilele wa Desemba, kufunguliwa kwa mazungumzo ya kujiunga na Ukraine, ambayo Viktor Orban pia aliyapinga, kuliwezekana kwa sababu wawakilishi hao walikubali kuondoka katika chumba hicho uamuzi ulipochukuliwa.

Katika mkesha wa mkutano huu, Tume ilikubali kutoa baadhi ya euro bilioni 10 za fedha zilizokusudiwa kwa Hungary na ambazo hadi sasa zimezuiwa, ikiweka mbele mageuzi yaliyofanywa na Budapest ili kuboresha uhuru wa majaji wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.