Pata taarifa kuu

Uturuki: Mlipuko wapiga karibu na makao makuu ya Bunge Ankara

Mlipuko mkubwa umepiga leo Jumapili Oktoba 1 asubuhi katika mji mkuu wa Uturuki Ankara, karibu na makao makuu ya Bunge, ambalo linatarajiwa kufungua kikao kipya cha shughuli zake wakati wa mchana, shirika la habari la AFP limeripoti. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uturuki imesema ni "shambulio la kigaidi" lililofanywa na watu wawili.

Vikosi vya usalama vya Uturuki vimetumwa Ankara karibu na Wizara ya Mambo ya Ndani, Jumapili Oktoba 1, 2023, baada ya shambulio lililofanywa asubuhi.
Vikosi vya usalama vya Uturuki vimetumwa Ankara karibu na Wizara ya Mambo ya Ndani, Jumapili Oktoba 1, 2023, baada ya shambulio lililofanywa asubuhi. REUTERS - CAGLA GURDOGAN
Matangazo ya kibiashara

"Magaidi wawili walionekana kwenye gari nyepesi ya kijeshi karibu saa 9:30 asubuhi (sawa na saa 8:30 asubuhi kwa saa za Afrika ya Kati) mbele ya lango la kuingilia la Kurugenzi Kuu ya Usalama ya Wizara yetu ya Mambo ya Ndani na kutekeleza shambulio la bomu ", imesema wizara hiyo, ambayo inabainisha kuwa mlipuko huo umejruhi maafisa wawili wa polisi, kulingana na tathmini ya awali.

Kulingana na vyombo vya habari vya Uturuki, urushianaji risasi pia ulisikika katika eneo unakopatikana makao makuu ya Bunge na wizara nyingi. Magari mengi ya polisi na ambulansi zimetumwa katika eneo hilo.

Taarifa zaidi zinakujia

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.