Pata taarifa kuu
MAZUNGUMZO-AMANI

UN: Mkutano Mkuu wafunguliwa katika muktadha wa mizozo mingi

Kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kilifunguliwa Jumanne Septemba 19, kwa hotuba kali kutoka kwa nchi wanachama, katika muktadha wa migogoro mingi ya kimataifa. Katikati ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alijitokeza kwa mara ya kwanza ana kwa ana kwenye jukwaa, muda mfupi baada ya hotuba ya mwenzake wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva. Lakini tahadhari pia inaelekezwa kwa Nagorno-Karabakh, ambapo Azerbaijan imezindua mashambulizi mapya.

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilifunguliwa Jumanne Septemba 19, kwa hotuba kadhaa kutoka kwa wakuu wa nchi, katika muktadha wa migogoro mingi, huko New York. Hapa, ni wakati wa hotuba ya Rais wa Marekani Joe Biden.
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilifunguliwa Jumanne Septemba 19, kwa hotuba kadhaa kutoka kwa wakuu wa nchi, katika muktadha wa migogoro mingi, huko New York. Hapa, ni wakati wa hotuba ya Rais wa Marekani Joe Biden. AP - Mary Altaffer
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alipanda jukwaa la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne kwa mara ya kwanza tangu uvamizi wa Urusi, mbele ya jumuiya ya kimataifa iliyogawanyika na kutikiswa na migogoro ya mfululizo, hasa vita vya Ukraine. Mwaka mmoja uliopita, aliidhinishwa kutoa hotua yake kupitia ujumbe wa video.

Wakati huu, anashiriki ana kwa ana, kwa kikao cha ngazi ya juu cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tangu siku ya Jumanne na mkutano maalum wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo Jumatano, kabla ya kuondoka kuelekea Washington ambako atapokelewa katika Ikulu ya Marekani siku ya Alhamisi. .

Zelensky anaishutumu Urusi kwa "mauaji ya halaiki" kwa kuteka nyara watoto wa Ukraine

Katika hotuba yake, Volodymyr Zelensky aliishutumu Urusi kwa "kutumia bei ya chakula (...) na nishati ya nyuklia kama silaha", akisema kwamba Moscow "haina haki ya kushikilia silaha za nyuklia", alisema hayo katika jukwaa la kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa New York, ambako alishangiliwa kwa muda mrefu.

Uhamisho wa Urusi wa "makumi ya maelfu" ya watoto wa Ukraine katika maeneo inayokalia nchini Ukraine ni "mauaji ya halaiki", alikashifu rais wa Ukraine, chini ya macho ya naibu balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa Dmitry Polyanskiy, aliyepo kwenye meza ya Urusi. “Tunajaribu kuwarudisha watoto hawa nyumbani, lakini muda unakwenda. Nini kitatokea kwao? Huko Urusi, wanafundishwa chuki ya Ukraine, na uhusiano wote na familia zao umekatwa. Haya ni mauaji ya kimbari ya waziwazi.”

Rais wa Ukraine, katika hotuba yake ya kwanza ya ana kwa ana kwa Bunge la Umoja wa Mataifa, alitangaza kuwa nchi yake inatayarisha "mkutano wa amani wa dunia" ambao anataka kuwaalika viongozi wote wa dunia wanaopinga "uvamizi" wa Ukraine unaofanywa na Urusi. “Majadiliano na mabadilishano muhimu yalifanyika Hiroshima, Copenhagen na Jeddah kuhusu utekelezaji wa mpango wa amani. Na tunatayarisha mkutano wa kilele wa amani duniani. Ninawaalika nyote - wale wote ambao hawaungi mkono uchokozi wowote - kuandaa kwa pamoja mkutano huu wa kilele," alisisitiza.

Rais huyo wa Ukraine anatarajiwa kukutana na mwenzake wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva siku ya Jumatano, baada ya kushindwa kukutana mwezi Mei wakati wa mkutano wa kilele wa G7, kwa mujibu wa ofisi ya rais wa Brazil. Tangu kuanza kwa vita nchini Ukraine, Brazil, ambayo iliunda kundi la Brics na Urusi, imekataa kusambaza silaha kwa Kiev au kuweka vikwazo dhidi ya Urusi ya Vladimir Putin. Rais wa Brazil alizua mzozo kwa kudai mara kwa mara kwamba jukumu la mzozo huo lilishirikiwa, hata kama alilaani uvamizi wa Urusi.

Lula kwa mara nyingine tena anataka "mazungumzo" kati ya Kyiv na Moscow

Wakati wa hotuba yake siku ya Jumanne kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, rais wa Brazil alitoa wito wa "mazungumzo" katika mzozo huo, akisema kwamba "kazi lazima ifanyike ili kuunda nafasi ya mazungumzo" kati ya pande zote. Lula alilalamika kwamba "mengi yamewekezwa katika silaha na kidogo sana katika maendeleo".

Vita vya Ukraine vinaonyesha kutoweza kwetu kwa pamoja kushikilia madhumuni na kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa. Hatupunguzii ugumu unaopatikana katika kupatikana kwa amani, lakini hakuna suluhu litakalodumu ikiwa halitokani na mazungumzo. Nilikariri kwamba tulihitaji kufanya kazi ili kuunda nafasi ya mazungumzo. (…) Utulivu na usalama hautahakikishwa pale ambapo kutengwa kwa jamii na ukosefu wa usawa unatawala. Umoja wa Mataifa ulizaliwa kuwa mahali pa kuelewana kupitia mazungumzo. Jumuiya ya kimataifa lazima ichague kati ya upanuzi wa migogoro, kuzorota kwa ukosefu wa usawa na mmomonyoko wa utawala wa sheria. Kwa upande mwingine, kufanywa upya kwa taasisi za kimataifa zinazojitolea kuendeleza amani.

Kwa upande wake, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan aliahidi "kuongeza" "juhudi" zake za kidiplomasia "kumaliza vita" nchini Ukraine iliyovamiwa na Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.