Pata taarifa kuu

Urusi yashutumu nchi za magharibi kwa 'kuvuruga' mkutano wa G20

Urusi imeshutumu nchi za Magharibi siku ya Jumamosi (Februari 25) kwa "kuvuruga" mkutano wa kilele wa Fedha wa G20 nchini India kwa kujaribu kuidhinisha taarifa ya pamoja kuhusu Ukraine, ambayo haikufanyika kwa sababu ya hitilafu.

Kulingana na Moscow, Marekani, EU na G7 "wamevuruga shughuli za kupitishwa kwa maamuzi ya pamoja" kwa kujaribu kulazimisha kuandkwa kwa baadhi ya maneno ili tafsiri yao ya mzozo wa Ukraine ionekane katika taarifa ya pamoja. Wizara imeshutumu Washington na washirika wake kwa kutoa 'makataa' kwa 'wajumbe wengi'.
Kulingana na Moscow, Marekani, EU na G7 "wamevuruga shughuli za kupitishwa kwa maamuzi ya pamoja" kwa kujaribu kulazimisha kuandkwa kwa baadhi ya maneno ili tafsiri yao ya mzozo wa Ukraine ionekane katika taarifa ya pamoja. Wizara imeshutumu Washington na washirika wake kwa kutoa 'makataa' kwa 'wajumbe wengi'. via REUTERS - PRESS INFORMATION BUREAU
Matangazo ya kibiashara

"Tunasikitika kwamba shughuli za G20 zinaendelea kuvurugwa na nchi za magharibi na kutumika kwa njia ya chuki dhidi ya Urusi na makabiliano kamili," Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imesema katika taarifa. 

Kulingana na Moscow, Marekani, EU na G7 "wamevuruga shughuli za kupitishwa kwa maamuzi ya pamoja" kwa kujaribu kulazimisha kuandkwa kwa baadhi ya maneno ili tafsiri yao ya mzozo wa Ukraine ionekane katika taarifa ya pamoja. Wizara imeshutumu Washington na washirika wake kwa kutoa 'makataa' kwa 'wajumbe wengi'.

"Tunazihimiza nchi za Magharibi kukataa sera yao ya uharibifu haraka iwezekanavyo, ili kutambua ukweli wa lengo la ulimwengu wa pande nyingi," Wizara ya mambo ya nje ya Urusi imeongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.