Pata taarifa kuu

Indonesia kupokea dola bilioni 20 ili kupunguza utegemezi wake kwa makaa ya mawe

Dola bilioni ishirini ndizo ambazo Indonesia inapaswa kupokea kutoka kwa kundi la nchi tajiri na taasisi za kimataifa ili kupunguza utegemezi wake kwa makaa ya mawe. Tangazo hilo limetolewa kando ya mkutano mkuu wa uchumi wa kundi al nchi tajiri, G20, kwenye kisiwa cha Bali nchini Indonesia. Miongoni mwa nchi zinazoshiriki: Marekani, Ufaransa, Canada na Uingereza.

Mlima wa makaa ya mawe unavutwa kwenye Mto Musi huko Palembang, Sumatra Kusini, Indonesia.
Mlima wa makaa ya mawe unavutwa kwenye Mto Musi huko Palembang, Sumatra Kusini, Indonesia. ©Antara Foto/Nova Wahyudi/ via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kutokana na makubaliano hayo, Indonesia, ambayo ni nchi ya nne kwa kuwa na watu wengi zaidi duniani yenye wakazi milioni 300, itaweza kufikisha lengo lake la kutoegemeza kaboni ifikapo mwaka 2050. Waziri wa Fedha wa Indonesia, anayehudhuria mkutano huo unaofanyika mjini Bali, ameelezea hatua hii kuwa ujumbe tosha na muhimu, sio tu katika Pasifiki, lakini ulimwenguni kote. Ufadhili unaopatikana kwa kipindi cha miaka mitatu hadi mitano hugawanywa kwa usawa kati ya sekta za umma na zile za kibinafsi, kwa njia ya misaada, dhamana ya mkopo au uwekezaji wa kibinafsi.

Makumi ya mamilioni ya Waindonesia wako katika hatari ya majanga ya asili kutokana na mabadiliko ya Tabia nchi, hasa wale wanaoishi katika maeneo ya mabondeni, ameongeza. Na kulingana na data ya kisayansi, nchi hii inaweza kupoteza zaidi ya visiwa 2,000 ifikapo mwaka 2030 kutokana na kuongezeka kwa viwango vya bahari.

Mpito wa haraka kwa nishati mbadala

Nyongeza hii itafanya uwezekano wa kufanya mpito kwa nishati mbadala kwa haraka zaidi. Serikali ya Indonesia tayari imetambua mitambo kadhaa ya nishati ya makaa ya mawe ambayo inaweza kuzimwa na kuwa na jumla ya pato la gigawati 15.

Mpango wa uwekezaji, uliotangazwa na Ikulu ya Marekani, unafuatia ahadi ya malipo mengine ya dola bilioni 98 kwa Afŕika Kusini, taifa la lililostawi kiviwanda barani Afŕika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.