Pata taarifa kuu

Serbia yajiandaa kupeleka vikosi vya kijeshi kwenye mpaka wa Kosovo

Tangu kukamatwa kwa afisa wa polisi wa zamani wa Serbia katikati ya mwezi wa Desemba, mamia ya watu wamekuwa wakiweka vizuizibarabarani kaskazini mwa Kosovo, kuelekea vituo viwili vya mpaka. Mnamo Jumapili, Septemba 25, hali ya wasiwasi iliongezeka na kuonekana kwa vizuizi vipya kulisikika milio ya risasi.

Wanajeshi wa jeshi la Serbia, Oktoba 20, 2021.
Wanajeshi wa jeshi la Serbia, Oktoba 20, 2021. © ANDREJ ISAKOVIC / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na Serbia, tukio hilo lilitokea wakati vikosi vya Kosovo vilijaribu kuvunja kizuizi karibu na eneo la Zubin Potok. Kile ambacho polisi wa Kosovo walikanusha. Kwa upande mwingine, anaelezea Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kosovar, wanajeshi wa kikosi cha kulinda amani cha Kosovo (Kfor) waliokuwa wakifanya doria walishambuliwa. Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kilikuwa katika eneo hilo, vinathibitisha vyombo vya habari vya ndani, lakini hakuna watu waliojeruhiwa au kutokea uharibifu wowote. Kfor imejizuia kuzungumza lolote.

Akijibu kwenye runinga ya Serbia, Jenerali Milan Mojsilovic ameelezea hali kuwa "tete" na akaeleza kuwa kuwepo kwa jeshi la Serbia sasa ni muhimu kwenye "mstari wa utawala", neno linalotumiwa nchini Serbia kutaja mpaka na Kosovo. Na kwamba mamlaka ya jeshi hapo itatekelezwa kikamilifu, bila hata hivyo kueleza kwa kina maudhui ya mamlaka hayo.

Vizuizi viliwekwa baada ya kukamatwa kwa afisa wa polisi wa zamani wa Serbia mnamo Desemba 10. Tukio hilo lilitokana na kukamatwa kwa afisa wa polisi wa zamani wa Serbia kwa njia isiyo ya moja kwa moja kutoka Mwezi Novemba, mgogoro kati ya pande hizo mbili kuhusu suala la usajili wa magari ya Waserbia ulihitaji upatanishi na Umoja wa Ulaya. Serbia inakataa kutambua uhuru wa Kosovo, ambayo inakaliwa zaidi na Waalbania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.