Pata taarifa kuu

Urusi: Uamuzi wa kununua mafuta ya Urusi, kwa Dola 60 kutatiza operesheni Ukraine

Urusi inasema, hatua ya mataifa ya G7 na Umoja wa Ulaya kuamua kununua mafuta yake ghafi Dola Sitini kwa kila pipa, hakutarudhisha nyuma na kutatiza operesheni zake nchini Ukraine, wakati huu nchi hiyo ikishuhudia kukatika kwa umeme na maji baada ya mashambulio ya Urusi, katika miji kadhaa. 

msemaji wa Ikulu ya Kremlin, Dmitry Peskov amesema uchumi wa Urusi ni imara inayowezesha kuendelea kwa operesheni maalum ya kijeshi nchini Ukraine.
msemaji wa Ikulu ya Kremlin, Dmitry Peskov amesema uchumi wa Urusi ni imara inayowezesha kuendelea kwa operesheni maalum ya kijeshi nchini Ukraine. AP - Alexander Zemlianichenko
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi wa kununua mafuta ya Urusi, kwa bei hiyo ya Dola 60 kwa pipa, ilifkiwa na mataifa hayo tajiri duniani, kwa lengo la kuinyima Urusi fursa ya kupata fedha za kuendelea kuishambulia Ukraine. 

Hata hivyo, msemaji wa Ikulu ya Kremlin, Dmitry Peskov amesema uchumi wa Urusi ni imara inayowezesha kuendelea kwa operesheni maalum ya kijeshi nchini Ukraine. 

Aidha, amesema  Urusi haitatambua bei hiyo ya Mataifa ya Magharibi, inayolenga kuyumbisha nchi hiyo ambayo ni ya pili kwa uzalishaji wa mafuta duniani. 

Licha ya kupongeza na kukaribisha hatua hii, Ukraine inasema haitoshi kuizuia Urusi kuendelea na uvamizi unaoendelea, hatua ambayo rais Volodymyr Zelensky amesema hatua ya mataifa hayo ni dhaifu. 

Katika hatua nyingine, kumekuwa na ongezeko la bei ya gesi, kufuatia hatua ya Urusi kusitisha usambazaji wa bidhaa hiyo barani Ulaya, baada ya kuwekewa vikwazo vya kiuchumi. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.