Pata taarifa kuu

Ukraine: Maji na umeme vyakatwa baada ya mashambulizi ya Urusi

Ving'ora vya onyo vimesikika kote nchini Ukraine Jumatatu, Desemba 5. Makombora ya Urusi yamedondoshwa kusini mwa nchi, huku mengine yakiharibiwa na mfumo wa ulinzi wa anga wa Ukraine. 

Wakazi wakikimbilia katika vituo vya treni za mwendo kasi kufuatia mashambulizi ya Urusi mnamo Desemba 5, 2022 huko Kyiv, Ukraine.
Wakazi wakikimbilia katika vituo vya treni za mwendo kasi kufuatia mashambulizi ya Urusi mnamo Desemba 5, 2022 huko Kyiv, Ukraine. © REUTERS - SHANNON STAPLETON
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi haya ya Urusi, ambayo yamesababisha vifo vya watu wasiopungua wawili kulingana na mamlaka za ndani, yalisababisha kukatika kwa umeme na maji katika miji kadhaa ya nchi.

Karibu saa saba na dakika kumi ving'ora vimesikika katikati mwa mji wa Kyiv, na kusababisha wakazi kutafuta makazi katika sehemu za chini ya ardhi.

Kulingana na vyanzo kadhaa, karibu makombora mia moja yalirushwa kuelekea Ukraine na ndege za Urusi, lakini pia kutoka baharini.

Hali inaonekana kuchukuliwa kwa uzito mkubwa na mamlaka ya Ukraine, wakati Ubalozi wa Ufaransa nchini Ukraine umetuma ujumbe kwa raia wa Ufaransa waliopo katika eneo hilo, ili kuwaonya kuhusu "shambulio kubwa la anga" nchini humo.

Haraka sana, mamia ya wakazi wa Kiev walikimbilia katika vituo vya treni za mwendo kasi vya mji mkuu, wakati nje kidogo ya jiji, milipuko imeripotiwa.

Katikati ya alasiri, mfumo wa ulinzi wa anga unaonekana kufanya kazi katika mji wa Kyiv kama katika mikoa kadhaa, ukiharibu makombora kadhaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.