Pata taarifa kuu

Ukraine yadai kupokea vifurushi vyenye macho ya wanyama kwenye balozi zake

Macho ya wanyama yalitumwa kwa balozi na balozi ndogo za Ukraine, siku chache baada ya wimbi la vifurushi vilivyopokelewa nchini Uhispania. Kyiv inasema, bila shaka, ni mpango wa Moscow.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky wakati wa kikao cha 77 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Septemba 21, 2022.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky wakati wa kikao cha 77 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Septemba 21, 2022. AFP - ANGELA WEISS
Matangazo ya kibiashara

Bahasha, iliyowekwa kwenye kioevu na ikiwa na harufu ya ajabu. Katika bahasha hiyo: macho ya wanyama. Hiki ni kifurushi kilichopokelewa na balozi kadhaa za Ukrainei huko Ulaya, kulingana na Kyiv.

"Vifurushi vya umwagaji damu viliwasili katika balozi za Hungary, Uholanzi, Poland, Croatia, Italia, Austria, ubalozi mdogo huko Naples na Krakow, na ubalozi mdogo huko Brno," msemaji wa diplomasia ya Ukraine Oleg Nikolenko amesema katika taarifa.

Kwa wakati huu, haiwezekani kutambua watumaji wa barua hizi. Lakini kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, anasema hakuna shaka: hili ni jaribio la vitisho vya Urusi. Anaishutumu Kremlin kwa kuendesha kampeni ya ugaidi iliyopangwa vyema huku Moscow ikikabiliwa na kushindwa mara kadhaa kijeshi katika wiki za hivi karibuni.

Na kwa siku chache zilizopita, Uhispania imekuwa ikilengwa na wimbi vifurushi. Ubalozi wa Ukraine, Wizara ya Ulinzi au kampuni ya silaha ilipokea barua zenye vilipuzi. Moja yao ilielekezwa moja kwa moja kwa Waziri Mkuu. Tena, haiwezekani kutambua asili ya usafirishaji huu.

Uhispania imeimarisha usalama wa tawala hizi na kutaja vitendo hivi kama vya kigaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.