Pata taarifa kuu

Uingereza: Liz Truss ateuliwa rasmi na Malkia Elizabeth II kuwa Waziri Mkuu

Lizz Truss, 47, anachukua nafasi ya Boris Johnson, ambaye alilazimika kujiuzulu baada ya kashfa.Malkia Elizabeth amemteua Liz Truss kama Waziri Mkuu wa Uingereza siku ya Jumanne, akiwa na dhamira ya kuiongoza nchi hiyo kupitia mdororo wa uchumi na nishati unaokaribia ambao unatishia mustakabali wa mamilioni ya kaya na biashara.

Malkia Elizabeth II anampokea Waziri Mkuu mpya Liz Truss huko Balmoral huko Scotland mnamo Septemba 6, 2022.
Malkia Elizabeth II anampokea Waziri Mkuu mpya Liz Truss huko Balmoral huko Scotland mnamo Septemba 6, 2022. © AP/Jane Barlow
Matangazo ya kibiashara

Bi Truss, Waziri Mkuu wa nne wa Tory katika kipindi cha miaka sita, alisafiri hadi katika eneo la familia ya kifalme huko Scotland kutwikwa jukumu na mfalme huyo mwenye umri wa miaka 96 kuunda serikali. Anachukua nafasi ya Boris Johnson, ambaye alilazimika kujiuzulu baada ya miaka mitatu ya misukosuko ya utawala wake.

"Malkia amempokea kwa mazungumzo Elizabeth Truss na kumtaka kuunda serikali mpya," ofisi ya mfalme imesema katika taarifa.

Uingereza, ambayo imekuwa ikiongozwa na Waconservative tangu 2010, imebadilika kutoka kwa shida moja hadi nyingine katika miaka ya hivi karibuni na matarajio ya muda mrefu wa dharura ya nishati yanakaribia, ambayo inaweza kuondoa akiba ya kaya na kutishia mustakabali wa biashara ndogo ndogo, ambazo bado zimelemewa na mikopo ya wakati wa COVID.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.