Pata taarifa kuu

EU yatoa mpango wa bei ya gesi ya Urusi

Wakati bei ya nishati ikiendelea kupanda, Tume ya Ulaya imewasilisha Jumatano, Septemba 7 njia zake za kupunguza bili za nishati za nchi wanacham wa Umoja wa Ulaya, ikiwa na kikomo cha bei ya gesi ya Urusi iliyoagizwa na umoja huo. 

Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Brussels kuhusu mpango wa nishati wa Ulaya, Septemba 7, 2022.
Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Brussels kuhusu mpango wa nishati wa Ulaya, Septemba 7, 2022. © Virginia Mayo / AP
Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati Rais wa Urusi Vladimir Putin ametishia Jumatano Septemba 7 kusitisha utoaji wote wa hidrokaboni ikiwa hatua kama hiyo itachukuliwa.

Katikati ya vita vya nishati, lengo la Umoja wa Ulaya bado ni "kupunguza mapato" yanayotumiwa na Kremlin "kufadhili mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Ukraine". Pendekezo hili la kupunguza bei ya gesi ya Urusi, hata hivyo, lina hatari ya kuchochea mvutano na Moscow: mamlaka ya Urusi inaweza kuacha kabisa utoaji wa gesi hata kabla ya nchi za Umoja wa Ulaya (EU) kuwa tayari kukabiliana nayo.

Shida nyingine, hata kama Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen amesema kwamba gesi ya Urusi sasa ni 9% tu ya gesi iliyoingizwa Ulaya, ikilinganishwa na 40% mwanzoni mwa vita nchini Ukraine:

Sote tunajua kwamba vikwazo vyetu vinapunguza kasi ya uchumi wa Urusi, na athari mbaya. Lakini Putin kwa sehemu anaipunguza kupitia mapato ya mafuta. Tunahitaji kukata mapato kutoka Urusi, ambayo Putin anaitumia kufadhili vita vyake vya ukatili nchini Ukraine. Na sasa kazi yetu ngumu katika miezi michache iliyopita inazaa matunda. Kwa sababu ukiangalia gesi iliyoagizwa kutoka nje mwanzoni mwa vita, 40% ilikuwa gesi ya Kirusi. Leo, tuko kwenye 9%.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.