Pata taarifa kuu

Zelensky atoa wito wa 'mwitikio mkali wa kimataifa' kufuatia shambulio Kramatorsk

Katika siku ya 45 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, hii Aprili 9, ni hasira ambayo inatawala baada ya shambulio lililohusishwa na Urusi siku ya Ijumaa dhidi ya kituo cha treni cha Kramatorsk, katika mji wa Donbass, shambulio ambalo limesababisha vifo vya watu hamsini, ikiwa ni pamoja na watoto watano.

Kipande cha kombora baada ya shambulio la Kramatorsk, Ijumaa Aprili 8, 2022.
Kipande cha kombora baada ya shambulio la Kramatorsk, Ijumaa Aprili 8, 2022. AP - Andriy Andriyenko
Matangazo ya kibiashara

Takriban watu hamsini waliuawa katika shambulio la roketi kwenye kituo cha treni cha Kramatorsk, huko Donbass, ambapo raia wanaendelea kutoroka eneo hili la mashariki mwa Ukraine. Moscow imekanusha kuhusika shambulio hilo na inalaani "uchochezi" wa vikosi vya Kyiv.

Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen alifanya mkutano na waandishi wa habari na Rais Zelensky baada ya kuzuru mji wa Kyiv na viunga vyake. Ursula von der Leyen alitangaza kwamba Ukraine ina "mustakabali wa Ulaya", wakati Urusi inatishiwa "kutengwa". Umoja wa Ulaya utafungua tena uwakilishi wake wa kidiplomasia mjini Kyiv.

Mamlaka ya Ukraine inajaribu kuwahamisha raia kutoka mashariki, wanaotishwa na mashambulizi ya Urusi, huku Rais Volodymyr Zelensky akisema kuwa uharibifu wa Borodyanka ni mbaya zaidi kuliko ule ulioonekana hivi karibuni karibu na mji mkuu baada ya kuondoka kwa vikosi vya Urusi.

Marufuku ya kutotoka nje itaanza kutumika kuanzia Jumamosi jioni hadi Jumatatu asubuhi huko Odessa, bandari kuu ya Ukraine kwenye Bahari Nyeusi, kutokana na "tishio" la mashambulio ya makombora, mamlaka ya eneo hilo imetangaza.

Mkoa wa Sumy, unaopakana na Urusi kaskazini-mashariki mwa Ukraine, "umekombolewa" kabisa kutoka kwa vikosi vya Urusi, mkuu wa utawala wa mkoa alitangaza Ijumaa, na kuongeza, hata hivyo, kwamba eneo hilo "halikuwa na uhakika" na kwamba operesheni ya kutengua mabomu inaendelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.