Pata taarifa kuu

Kituo cha treni mashariki mwa Ukraine chashambulia, karibu raia 50 wauawa

Katika siku ya 44 ya uvamizi wa Ukraine nchini Ukraine, Aprili 8, fuata habari za hivi punde za mzozo huo moja kwa moja. Wakati Ukraine ikihangaika kuwahamisha raia mashariki mwa nchi hiyo, Urusi imetekeleza shambulizi lililosababisha vifo vya takriban watu 50 wakiwemo watoto watano huko Kramatorsk siku ya Ijumaa asubuhi.

Wanajeshi wa Ukraine wakiwa wamebeba waathiriwa baada ya shambulio la bomu katika kituo cha treni katika jiji la mashariki mwa Ukraine la Kramatorsk, katika mkoa wa Donbass, Aprili 8, 2022.
Wanajeshi wa Ukraine wakiwa wamebeba waathiriwa baada ya shambulio la bomu katika kituo cha treni katika jiji la mashariki mwa Ukraine la Kramatorsk, katika mkoa wa Donbass, Aprili 8, 2022. AFP - HERVE BAR
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo, Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen na mkuu wa diplomasia ya Ulaya Josep Borrell wanatarajia kuzuru Kyiv, ishara ya Ukraine kuungwa mkono dhidi ya uvamizi wa Urusi.

Hayo yanajiri wakati Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen anatarajiwa mjini Kyiv Ijumaa hii kueleza "uungaji mkono wake usioyumbayumba" kwa Ukraine katika mapambano yake dhidi ya uvamizi wa Urusi.

Makumi ya watu waliuawa katika shambulio la roketi kwenye kituo cha Kramatorsk huko Donbass, ambapo raia wanaharakia kutoroka eneo hili la mashariki mwa Ukraine. Moscow imekanusha kuhusika shambulizi hilo na inashutumu "uchochezi" wa vikosi vya Kyiv.

Mamlaka ya Ukraine inajaribu kuwahamisha raia kutoka mashariki, wanaotishwa na mashambulizi ya Urusi, huku Rais Volodymyr Zelensky akisema kuwa uharibifu wa Borodyanka ni mbaya zaidi kuliko ule ulioonekana hivi karibuni karibu na mji mkuu baada ya kuondoka kwa vikosi vya Urusi.

Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amewasili Bucha, mji mdogo kaskazini magharibi mwa Kyiv ambao umekuwa ishara ya ukatili wa vita nchini Ukraine, kulingana na shirika la habari la AFP.

Ursula von der Leyen, ambaye ameandamana na mkuu wa diplomasia ya Ulaya, Josep Borrell, ametangaza siku ya Ijumaa kwamba atakwenda mji mkuu kama ishara ya kuunga mkono Ukraine. Viongozi hao wawili wameenda kuona makaburi ya halaiki yaliyochimbwa huko Bucha ili kuzika makumi ya raia waliouawa katika mapigano hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.