Pata taarifa kuu

Miili ya Wakurdi 16, wahanga wa ajali ya meli nchini Uingereza, yarejeshwa makwao

Ilikuwa Novemba 24, zaidi ya mwezi mmoja uliopita: watu 27 walipoteza maisha katika ajali ya meli iliyozama katika bahari ya Uingereza. Walikuwa wakijaribu kuingia Uingereza kutoka pwani ya Ufaransa. Miongoni mwao walikuwa Wakurdi 16 kutoka Iraq. Baada ya kusubiri kwa muda mrefu kwa familia, miili ya wahanga imerejeshwa makwao usiku wa kuamkia leo Jumapili.

Picha iliyopigwa Soran, kaskazini mwa Iraq, katika chumba cha kulala cha Maryam Nuri Hama Amin, mmoja wa wahanga wa ajali ya boti iliyozama Novemba 24, 2021.
Picha iliyopigwa Soran, kaskazini mwa Iraq, katika chumba cha kulala cha Maryam Nuri Hama Amin, mmoja wa wahanga wa ajali ya boti iliyozama Novemba 24, 2021. Safin HAMED AFP
Matangazo ya kibiashara

Saa mbili asubuhi, ndege iliyokuwa imebebea miili ya wahanga hao ilitua kwenye uwanja wa ndege wa Erbil nchini Iraq. Ndani ya ndege hiyo, miili ya wahanga 16, wanaume kumi, wanawake wanne, kijana na msichana mwenye umri wa miaka saba.

Ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu walionekana kwenye uwanja wa ndege wakija kupokea miili ya wapendwa wao.

Iliposhushwa kwenye ndege, majeneza yaliwekwa katika magari ya wagonjwa na kuanza safari kuelekea miji ya Darbandikhan, Ranya, Soran na Qadrawa. katika miji yao hiyo ya asili, ndiko ambapo wahanga watazikwa.

Lakini kabla ya kuomboleza, maswali kadhaa yamesalia kwa familia kuhusu kile kilichotokea usiku huo wa Novemba 23, 2021, na hasa kuhusu maombi haya ya usaidizi ambayo wahamiaji wanadaiwa kutoa kwa mamlaka ya Ufaransa na Uingereza.

Mmoja wa walionusurika alisema hawakujibiwa.

"Hakuna ombi lililotolewa," imejibu wilaya ya Manche kwa upande wa Ufaransa.

Mahakama ya Ufaransa inaweza kwa vyovyote vile kutangaza uamuzi wake. Wiki iliyopita, chama cha Utopia 56 kiliwasilisha malalamishi ya "mauaji" na "kushindwa kutoa msaada" dhidi ya gavana na maafisa wa idara ya dharura kutoka Ufaransa na Uingereza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.