Pata taarifa kuu
LIBYA-USALAMA

Madaktari wasio na mipaka wagundua maiti kumi za wahamiaji kwenye pwani ya Libya

Maiti kumi za wahamiaji, ambao huenda walikosa hewa hadi kufariki dunia, zimegunduliwa ndani ya boti iliyojaa mizigo nje ya pwani ya Libya, Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) limetangaza. Meli ya misaada ya shirika la Geo Barents, imeokoa manusura 99.

Wahamiaji waliokolewa na shirika la MSF katika bahari ya Mediterania Septemba 20, 2021.
Wahamiaji waliokolewa na shirika la MSF katika bahari ya Mediterania Septemba 20, 2021. © AP Photo/Ahmed Hatem
Matangazo ya kibiashara

"Chini ya boti ya mbao iliyojaa kupita kiasi, watu kumi walipatikana wamekufa," MSF imeandika kwenye ukurasa wake Twitter. Vifo 10 vinavyozuilika (...) Watu 10 waliofariki dunia kwa kukosa hewa, baada ya masaa 13 ya kusafiri baharini. Njia mbaya zaidi katika Bahari ya Mediterania. Je, watu wanawezaje kukubali hili katika mwaka  2021? "

Mtoto wa miezi kumi katika boti

Makumi ya maelfu ya watu wanajaribu kuwasili Ulaya kwa kuvuka bahari ya Mediterania kutoka Libya au Tunisia ili kufika Italia. Njia hii ni hatari sana: takriban watu 1,236 tayari wameangamia mwaka huu walipokuwa wakijaribu kutumia njia hii, dhidi ya watu 858 katika kipindi kama hicho mwaka 2020, kwa mujibu wa Flavio Di Giacomo wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IMO).

Operesheni ya uokoaji ya Geo Barents "pengine iliwaepusha waathiriwa wengine", ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, akisisitiza "haja ya kuimarisha doria baharini". Kwa mujibu wa MSF, Geo Barents kwa sasa inasafirisha watu 186, wakiwemo wanawake na watoto, mdogo akiwa na umri wa miezi 10. Shirika hili limeomba kuwe na bandari salama ili kuweza kuegesha na watu hao waweze kupokelewa na kuhudumiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.