Pata taarifa kuu

Antony Blinken ziarani Mexico kuimarisha ushirikiano

Hatua mpya katika uhusiano kati ya Marekani na Mexico, wamesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na mwenzake wa Mexico Marcelo Ebrard walitangaza Ijumaa, Oktoba 8.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken katika mkutano na waandishi wa habari huko Mexico Oktoba 8, 2021.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken katika mkutano na waandishi wa habari huko Mexico Oktoba 8, 2021. AP - Patrick Semansky
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alielezea mkakati mpya wa pamoja wa kupambana na uhalifu na biashara haramu ya binadamu. Wakati wa ziara hiyo nchini Mexico, wahamiaji 652 kutoka Amerika ya Kati walikuwa wamekamatwa wakiwa kwenye malori.

Kati ya wahamiaji 652 wa Amerika ya Kati waliokamatwa, zaidi ya nusu walikuwa watoto. Walikuwa wakisafiri kwa malori kilomita mia kadhaa kutoka mpaka kati ya nchi hizo mbili, kuelekea mji wa Monterrey kaskazini mwa Mexico. Madereva wanne walikamatwa.

Kwenye mpango wa uhamiaji, ushirikiano kati ya Mexico na Marekani unaimarika, amebaini Profesa Raul Benitez, wa kituo cha utafiti cha Amerika Kaskazini cha Chuo Kikuu cha Mexico, kwenye katika mahojiano na Aida Palau, wa Idhaa ya Kihispania ya RFI. "Serikali ya Mexico, kwa makubaliano na Marekani, inakataza wahamiaji kusafiri kwa basi nchini Mexico ikiwa hawana karatasi sahihi. Kwa hivyo kwa kuwa magari mengi makubwa yanayokuja kna bidhaa nchini Mexico hurejea tupu kwenda Marekani, na hivyo huchukuwa wahamiaji. "

Hii ni ziara ya pili nchini Mexico kwa afisa wa ngazi ya juu wa Marekani tangu kuapishwa kwa Rris Joe Biden mwezi Januari, baada ya ziara ya Makamu wa Rais Kamala Harris mwezi Juni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.