Pata taarifa kuu
MEXICO-USALAMA

Watu zaidi ya 30 wajeruhiwa katika makabiliano kati ya wahamiaji na polisi Mexico

Nchini Mexico, watu 17 wakiwemo maafisa 13 wa polisi wamejeruhiwa katika makabiliano kati ya vikosi vya usalama na msafara wa wahamiaji. Matukio hayo yalitokea kwenye lango la kuingia nchini Mexico, huku wahamiaji hao wakitaka kwenda kufanya Hija.

Wahamiaji wengi walitaka kushiriki katika Hija katika kanisa kuu ya huko Guadalupe kabla ya kuzuiwa na polisi, Desemba 13, 2021.
Wahamiaji wengi walitaka kushiriki katika Hija katika kanisa kuu ya huko Guadalupe kabla ya kuzuiwa na polisi, Desemba 13, 2021. © AP - Ginnette Riquelme
Matangazo ya kibiashara

Wahamiaji hawa, kutoka nchi za Salvador, Honduras na Haiti walitoka katika kijiji cha Rio Frio, kusini mwa Mexico. Walitaka kwenda kwenye kanisa kuu ya Guadalupe, kaskazini mwa mji mkuu, kushiriki katika ibada ya Hija ambayo imeleta pamoja mamia kwa maelfu ya watu katika siku za hivi karibuni.

"Walitutendea kama mbwa"

Walikataa ombi la serikali ya Mexico la kwenda sehemu mmoja, na walipofika karibu na daraja la Concorde, walijikuta wakizuiwa na mamia ya maofisa wa polisi. Makabiliano yalianza, mabomu ya machozi dhidi ya mawe. "Walitutendea kama mbwa," amesema mtetezi wa haki za wahamiaji aliyeandamana nao.

Serikali ya Mexico, kwa upande wake, inadai kwamba polisi iliwarudisha nyuma wahamiaji.

Mabasi yakodishwa

Mpema mchana, mabasi sita hatimaye yalikodishwa ili kuwapeleka wahamiaji hao kwenye kanisa kuu. Mapigano hayo yanakuja siku tatu baada ya ajali ya barabarani iliyowaua wahamiaji 55 Alhamisi ya wiki iliyopita.

Tangu kuzinduliwa upya kwa mpango wa "Kaa Mexico" na Mahakama ya Juu ya Marekani, wahamiaji wamelazimika kusubiri nchini Mexico kwa kusubiri matokeo ya madai yao ya kuomba hifadhi nchini Marekani. Lakini makabiliano mengine kati ya wahamiaji na vikosi vya usalama tayari yamefanyika katika miezi ya hivi karibuni kusini mwa mji mkuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.