Pata taarifa kuu
UINGEREZA-USHIRIKIANO

London yatoa leseni 23 za ziada baada ya kutishiwa na Paris

Uingereza imetoa leseni 23 za ziada kwa wavuvi wa Ufaransa, London na Brussels wametangaza Jumamosi hii, Desemba 11, siku moja baada ya tarehe ya mwisho iliyowekwa na Paris kutatua mzozo wa haki za uvuvi baada ya Uingereza kutoka katika Umoja wa Ulaya (Brexit).

Boti la wavuvi la Ufaransa likiwa mbele ya Saint-Hélier, kisiwa cha Jersey.
Boti la wavuvi la Ufaransa likiwa mbele ya Saint-Hélier, kisiwa cha Jersey. AFP - SAMEER AL-DOUMY
Matangazo ya kibiashara

Idadi hiyo inasalia chini sana ya leseni 104 zilizokuwa zikidaiwa na Ufaransa katika siku za hivi karibuni, ikitishia kufunguwa mashitaka ifikapo Ijumaa hii, Desemba 10,hhi ikiwa ni "ishara ya nia njema" kwa upande wa London.

"Jana jioni, baada ya kupokea ushahidi wa ziada wa kuunga mkono kutoka kwa Tume ya Ulaya, Uingereza ilitoa leseni 18 kwa meli zitakazobadilishwa" kuchukua nafasi ya meli zilizokuwa zikivua hapo awali katika maji ya Uingereza, msemaji wa serikali ya Uingereza amebaini.

Tangazo hili limethibitishwa na Tume ya Ulaya, ambayo inajadiliana kwa niaba ya Ufaransa. "Kazi ya kina zaidi ya kiufundi inaendelea kuhusu maombi saba ya ziada ya leseni kwa meli nyingine, na inatarajiwa kuhitimishwa Jumatatu," msemaji wa serikali ya Uingereza ameongeza.

Aidha, kisiwa cha Anglo-Norman cha Jersey, ambacho kinatoa leseni zake kwa kujitegemea, kimeidhinisha leseni tano mpya kwa wavuvi wa Ufaransa siku ya Jumamosi, ameongeza. Kulingana na Amesema maamuzi haya "yanahitimisha kipindi cha mazungumzo ya kina" ya siku chache zilizopita kati ya London na Tume ya Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.