Pata taarifa kuu

Suala la wahamiaji lazua mvutano mkubwa kati ya Ufarasa na Uingereza

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, amekasirishwa na kauli ya Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, kuwa Ufaransa iwachukue wahamiaji wanaokwenda nchini Uingereza.

Siku ya Alhamisi tarehe 25 Novemba, Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson aliiomba Ufaransa iwarudishe wahamiaji haramu ambao wangeweza kufika katika ufuo wa Uingereza, na HIVYO kusababisha hasira ya Paris.
Siku ya Alhamisi tarehe 25 Novemba, Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson aliiomba Ufaransa iwarudishe wahamiaji haramu ambao wangeweza kufika katika ufuo wa Uingereza, na HIVYO kusababisha hasira ya Paris. ANDY BUCHANAN AFP
Matangazo ya kibiashara

Macron amemwambia Boris kuwa, awe makini baada ya watu 27 kupoteza maisha katika eneo la bahari kati ya nchi hizo mbili.

Uhusiano wa mataifa haya mawili, umekuwa ukiyumba, kufuatia kulaumiana kwa wakimbizi lakini pia haki ya wavuvi katika eneo la Bahari kati ya nchi hizo mbili baada ya Uingereza kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya.

Mkutano uliopangwa kufanyika kati ya mawaziri wa Ulaya utafanyika Jumapili, Novemba 28 mjini Calais ili kujaribu kuvunja mkwamo huo. Lakini bila Uingereza. Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Gerald Darmanin alifuta mwaliko huo kwa Waingereza. Sababu ya mzozo huu: matamshi yaliyotolewa na Boris Johnson akiomba Ufaransa kuwarudisha wahamiaji wanaowasili Uingereza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.