Pata taarifa kuu

Mkutano wa kilele wa G20 kujadili masuala ya tabia nchi, Covid na uchumi wa dunia

Mkutano wa kilele wa nchi zilizostawi kiuchumi na kiviwanda, G20, umefunguliwa mjini Roma Jumamosi hii, Oktoba 30 ambapo wakuu wa nchi na serikali za nchi wanachama wanashiriki kujadili na kutafutia suluhu masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na tabia nchi, covid na uchumi wa dunia.

Roma, Oktoba 30, 2021: viongozi wa nchi zilizostawi kiviwanda, G20, wamewasili mjini Roma Italia, kuhudhuria mkutano wa kilele, ambao ni wa kwanza wa uso kwa uso tangu kuzuka kwa mripuko wa virusi vya Corona.
Roma, Oktoba 30, 2021: viongozi wa nchi zilizostawi kiviwanda, G20, wamewasili mjini Roma Italia, kuhudhuria mkutano wa kilele, ambao ni wa kwanza wa uso kwa uso tangu kuzuka kwa mripuko wa virusi vya Corona. REUTERS - YARA NARDI
Matangazo ya kibiashara

Mkutano wa Cop 26 utaanza Jumatatu huko Glasgow kujadili ongezeko la joto duniani, -baada ya mkutano wa G20-, ambao unatarajia kujadili mapambano dhidi ya janga la Covid-19 na ufufuaji wa uchumi wa dunia.

Viongozi hawa wanakabiliwa na shinikizo la kutafuta suluhisho linalofaa kushughulikia kadhia ya mabadiliko ya tabianchi, kuelekea mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuongezeka kwa joto duniani, utakaofanyika mjini Glasgow, Scotland kuanzia Jumapili.

Huu ni mkutano wa kwanza wa uso kwa uso kwa viongozi hawa tangu kuzuka kwa mripuko wa virusi vya Corona.

Mkutano huo unakuja, huku kukiwa na onyo kali kwa siku zijazo ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa.

Kundi hilo pia linatarajiwa kuidhinisha kiwango cha chini cha ushuru wa shirika duniani cha angalau 15%, ambacho kinaungwa mkono na nchi 140 kote ulimwenguni.

Mbali na faili zilizotajwa hapo awali, itakuwa pia, suala la kuzinduliwa tena kwa mpango wa nyuklia wa Iran wakati wa mkutano kati ya Marais wa Marekani Joe Biden wa Ufaransa Emmanuel Macron, na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson.

Ni "mkutano muhimu wa pande nyingi", Emmanuel Macron alisisitiza jana na hii G20 huko Roma lazima iwe "ya matokeo na ufanisi", ameripoti mwandishi wetu maalum, Valérie Gas. Rais wa Ufaransa, ambaye alitaja hasa mshikamano na Afrika kwa chanjo, na mabadiliko ya tabia nchi, yuko Roma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.