Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN

G20 kuisaidia Afghanistan kuimarisha uchumi wake

Nchi za G20 zenye uchumi mkubwa duniani, zimeahidi kuisaidia nchi ya Afghanistan kupambana na hali ngumu ya kiuchumi inayoshuhudiwa kwa sasa.

Umoja wa Ulaya umesema kuwa utatoa msaada wa Dola Bilioni 1.15 kwa ajili ya watu wa Afganistan lakini pia, kuwapokea wakimbizi.
Umoja wa Ulaya umesema kuwa utatoa msaada wa Dola Bilioni 1.15 kwa ajili ya watu wa Afganistan lakini pia, kuwapokea wakimbizi. WAKIL KOHSAR AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika kikao cha viongozi hao kupitia mtandao, viongozi hao wametoa hakikisho hili, wakati huu Umoja wa Mataifa ukizitaka nchi hizo tajiri kutoa msaada wa Mabilioni ya Dola, kuisaidia kuimarisha Uchumi wa taifa hilo.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, amesema nchi ya Afganistan isiachwe kuingia kwenye machafuko zaidi huku akisema nchi yake itatoa Euro Milioni 600 kwa nchi hiyo.

Naye rais wa Marekani Joe Biden amesema, msaada wowote kwa Afganistan unastahili kutolewa kupitia Mashirika huru ya Kimataifa na sio kundi la Taliban ili kuwasaidia wananchi wa Afganistan.

Tayari Umoja wa Ulaya umesema kuwa utatoa msaada wa Dola Bilioni 1.15 kwa ajili ya watu wa Afganistan lakini pia, kuwapokea wakimbizi.

Mwishoni mwa mwezi Agosti, Marekani iliondoa wanajeshi wake nchini Afganistan baada ya kuwa nchi hiyo kwa muda wa miaka 20.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.