Pata taarifa kuu
UFARANSA

Watoto 216,000 wafanyiwa udhalilishaji wa kijinsia Ufaransa

Tume huru kuhusu unyanyasaji wa kijinsia katika Kanisa (Ciase) nchini Ufaransa imebaini kuwa watoto wasiopungua 216,000 walikuwa wahanga wa vitendo kama hivyo tangu mwaka 1950. Kati ya viongozi wa kidini 2,900 na 3,200 wanatuhumiwa kwa unyanyasaji wa kijinsia.

Kati ya viongozi wa kidini 2,900 na 3,200 wanatuhumiwa kwa unyanyasaji wa kijinsia, imebaini ripoti ya CIASE.
Kati ya viongozi wa kidini 2,900 na 3,200 wanatuhumiwa kwa unyanyasaji wa kijinsia, imebaini ripoti ya CIASE. AFP - PETER MUHLY
Matangazo ya kibiashara

CIASE katika ripoti yake imefichua kuwa watoto wapatao 216,000 wamekuwa wakinyanyaswa kingono katika kanisa katoliki la Ufaransa kwa zaidi ya miaka 70 iliyopita. Baadhi ya watu 216,000 wamefanyiwa ukatili au unyanyasaji wa kijinsia na viongozi wa kanisa Katolika nchini Ufaransa walipokuwa watoto.

Waathiriwa wafikia hadi 330,000

Takwimu ambayo imeongezeka hadi 330,000 ikiongezwa idadi ya watoto waliofanyiwa vitendo hivyo vya ukatili na viongozi wa kidini wanaofanya kazi katika taasisi za Kanisa Katoliki, kama vile makasisi au makundi ya vijana. Na shida haifikiria kutatuliwa, kulingana na rais wa Tume hii.

Mkuu wa tume iliyotoa ripoti hiyo Jean-Marc Sauve amesema idadi hiyo ya watoto walionyanyaswa kingono, kulingana na utafiti wa kisayansi, inahusisha unyanyasaji uliofanywa na mapadri, makasisi pamoja na wafanyikazi wa kawaida katika kanisa hilo.

Ufichuzi huo ni wa hivi karibuni kulitikisa Kanisa Katoliki baada ya kuzongwa na kashfa za unyanyasaji wa kingono kote duniani, mara nyingi zikihusisha watoto, kwa zaidi ya miaka 20 iliyopita.

Jean-Marc Sauve, mkuu wa tume iliyotoa ripoti hiyo, aliiwasilisha hadharani ripoti yenyewe na kusema unyanyasaji huo ulikuwa ni wa kimfumo.

Papa Francis asikitishwa na ukatili dhidi ya watoto

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Ulimwenguni, Papa Francis, ameelezea masikitiko yake makubwa kwa wahanga wa dhuluma za kingono uliotendwa na uongozi wa kanisa hilo nchini Ufaransa, baada ya kuchapishwa hivi leo ripoti ya uchunguzi wa matukio hayo.

Msemaji wa Vatican, Matteo Bruni, amesema kiongozi huyo amehuzunishwa sana na matokeo ya uchunguzi huo huru, ambao umegunduwa kuwa viongozi wa kanisa lake waliwanyanyasa kingono jumla ya watoto 216,000 ndani ya kipindi cha miongo saba, kuanzia mwaka 1950, na kisha wakaufunika uovu huo, kwa kile alichokiita "veli la ukimya".

Bruni amesema Papa Francis anawalilia kwanza wahanga kwa majeraha yao na anawashukuru kwa ujasiri wa kujitokeza hadharani kuzungumzia dhulma waliofanyiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.