Kukamatwa kwa Carles Puigdemont: Mchakato wa maridhiano wawekwa hatarini
Tukio la kukamatwa kwa Carles Puigdemont huko Sardinia nchini Italia Alhamisi tarehe 23 Septemba imezua mtafaruku katika serikali kuu ya Pedro Sánchez. Tukio hili linaweza kuhatarisha mchakato wa mazungumzo ya wazi kati ya Waziri Mkuu wa Uhispania na serikali ya Barcelona.
Imechapishwa:
Hayo yanajiri wakati viongozi wa Italia wameamua kumuachilia Carles Puigdemont na kusema kuwa yuko huru kuondoka nchini humo au kubaki.
Kwa upande wake, chama cha mrengo wa kulia, kimeghadhabishwa na hatua hiyo ya Italia ya kumuachilia huru kiongozi huyo wa zamani wa Catalonia.
Habari za kukamatwa kwa Carles Puigdemont huko Sardinia Alhamisi jioni zilimshangaza kiongozi wa serikali kuu Pedro Sánchez. Na hali hii, haifanyi mambo kuwa rahisi kwake, ameripoti mwandishi wetu François Musseau kutoka Madrid.
Pedro Sánchez alianzisha mchakato wa mazungumzo na utawala unaotaka kujitenga wa Barcelona. Lengo ni kuboresha maridhiano na utawala wa Barcelona, kufikia makubaliano juu ya miradi mikubwa ya uwekezaji huko Catalonia, kuboresha aina ya ushuru katika jimbo hilo.