Pata taarifa kuu
UHISPANIA-CATALONIA-SIASA

Catalonia kukumbwa na maandamano makubwa

Maelfu ya waandamanaji wanatarajia kumiminika katika mitaa ya Barcelona leo Jumatano, miaka miwili baada ya jaribio la Catalonia kujitenga na Uhispania.

Waandamanaji wakiwa katika maandamano Barcelona, Septemba 11, 2018.
Waandamanaji wakiwa katika maandamano Barcelona, Septemba 11, 2018. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati hukumu dhidi ya viongozi wao inasubiriwa kutolewa mnamo mwezi Oktoba mwaka huu.

Tangu mwaka wa 2012, waandamanaji wanaotaka jimbo la Catalonia kujitenga na Uhispania, wamekuwa wakifanya maandamano makubwa kila tarehe 11 Septemba, siku ya "Diada", sikukuu ya Catalonia inayoadhimisha kumbukumu ya kudhibiti mji wa Barcelona mnamo mwaka 1714 dhidi ya askari wa Philip wa 5 wakati wa Vita vya Uhispania.

Watu zaidi ya milioni moja wamekuwa wakishiriki katika maandamano ya miaka ya hivi karibuni.

Maandamano ya leo yanatarajiwa kuanza saa 11:14 jioni.

Viongozi wa zamani wa Catalonia wanakabiliwa na kifungo cha maisha hadi miaka 25 jela.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.