Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO-SIASA

Uingereza: Wabunge saba wa chama cha Labour wajiuzulu

Wabunge saba kutoka chama kikuu cha upinzani nchini Uingereza cha Labour ambao hawakubaliani na kiongozi wao Jeremy Corbyn kuhusu Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya na vita dhidi ya ubaguzi, wamejiuzulu Jumatatu wiki hii.

Wabunge saba wa chama cha Laabour ambao wameamua kujiuzulu, Februari 18 London.
Wabunge saba wa chama cha Laabour ambao wameamua kujiuzulu, Februari 18 London. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa wabunge waliojiuzulu ambao wanadai kuwa wanaunda "kundi lisiloegemea" ni pamoja na Chuka Umunna, ambaye ameonekana kuwa  mpinzani na uongozi wa chama cha Labour na Luciana Berger, ambaye anakosoa mwenendo wa chama chake kwa vita dhidi ya ubaguzi. Hata hivyo Jeremy Corbyn amesema anasikitishwa na uamuzi wa wabunge hao.

Kundi hili la wabunge saba lilikuwa likimuitisha, wiki moja sasa, kubadili kuhusu mkakati na kufanya kampeni kwa kura ya pili ya maoni kuhusu kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Kujiuzulu kwa wabunge hawa kunaweza kusababisha mgawanyiko mkubwa katika chama hiki cha Labour, kwa mujibu wa chanzo kilio karibu na chama cha Labour.

Jeremy Corbyn hajakataa kura ya pili ya maoni ikiwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May, atashindwa kupata saini ya mkataba uliofikiwa na Brussels katika Bunge, lakini ameomba kwanza kufanyike uchaguzi wa mapema.

Pia ameongeza hoja ya kuepo kwa umoja wa kudumu wa forodha na EU, hoja ambayo mpaka sasa Waziri Mkuu amekuwa akipinga.

Baadhi ya wabunge wanamshtumu kutowajibika vilivyo katika vita dhidi ya ubaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.