Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO

Mpango mbadala wa Theresa May ni kuendelea na mpango wa awali

Siku sita baada ya mpango wake wa kujiondoa Umoja wa Ulaya kufutiliwa mbali na idadi kubwa ya wabunge, Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May amesema kuwa anajaribu kuondokana na sintofahamu hiyo na kutafuta makubaliano mapya na EU.

Theresa May akijitetea mbele ya wabunge Jumapili 21 kuhusu mpango wake wa Uingereza kujitoa Uoja wa Ulaya.
Theresa May akijitetea mbele ya wabunge Jumapili 21 kuhusu mpango wake wa Uingereza kujitoa Uoja wa Ulaya. UK Parliament
Matangazo ya kibiashara

Mpango huo umejikita katika suala la mpaka baina ya Ireland na Ireland ya Kasakazini.

Mwishoni mwa wiki May alilieleza baraza la mawaziri kuwa mpango wake mpya unasaka makubaliano na Umoja wa Ulaya juu ya suala la mpaka wa Ireland na kisha ataupeleka kwenye Baraza la chini la bunge la Uingereza wiki zijazo.

May amewaeleza wabunge kuwa kukataliwa kwa mpango wake wiki iliyopita, ilikuwa ni ishara kwamba serikali inapaswa kuchukua mwelekeo mpya kuhusu Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya na imefanya hivyo.

Ikiwa zimesalia wiki kumi ili kukamilika kwa muda wa Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya, Machi 29 saa tano usiku, mpaka sasa hakuna makubaliano yaliyoafikiwa huko London kuhusu mchakato huo.

Bi May amekataa kukubali kuwa Uingereza inaweza kuondoka Umoja wa Ulaya bila ya makubaliano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.