Pata taarifa kuu
AUSTRALIA-KANISA-HAKI

Kardinali Pell akabiliwa na kesi ya unyanyasaji wa kijinsia

Kardinali George Pell, mmoja wa washauri wa karibu wa kiongozi wa kanisa Katoliki dudiani Papa Francis, ni mwakilishi wa juu wa kanisa hilo ambaye anakabiliwa na kesi ya unyanyasaji wa kijinsia.

Kardinali George Pell akiondoka mahakamani huko Melbourne, Mei 1, 2018
Kardinali George Pell akiondoka mahakamani huko Melbourne, Mei 1, 2018 AFP
Matangazo ya kibiashara

Kardinali huyo, mwenye umri wa miaka 76, hakuvumiliwa kusumbuliwa wakati mahakama ya Melbourne imeamuru Jumannee hii ahukumiwe kwa mashtaka "mengi," huku yakiachwa zaidi ya nusu ya mashtaka, ikiwa ni pamoja na mashtaka makubwa zaidi.

"Sina hatia," Askofu Pell amejibu kwa sauti kubwa na bila kusita wakati mahakama ilimwuliza jinsi atajitetea mwenyewe, na hivyo kuthibitisha nafasi aliyokuwa nayo tangu wakati kesi hiyo iliibuka.

Baada ya kusoma uamuzi wake, Jaji Belinda Wallington amesema "amekubali" kiongozi huyo kufikishwa mahakamani kutoakana na kuepo kwa ushahidi wa kutosha ili kujibu "mashitaka mengi" yanayomkabili. Majaji watakutana Jumatano wiki hii kujadili tarehe ya kesi.

Kardinali, Pell ambaye alikuwa amewasili mahakamani chini ya ulinzi wa polisi wengi, ameachiliwa huru kwa dhamana. Amepigwa marufuku kuondoka Australia na tayari amekabidhi pasipoti yake kwa mamlaka husika, kwa mujibu wa mahakama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.