Pata taarifa kuu
UFARANSA-MATEKA-USALAMA

Mateka wa Ufaransa nchini Yemen, Isabelle Prime, yuko huru

Raia wa Ufaransa Isabelle Prime, aliyetekwa nyara nchini Yemen tangu mwezi Februari mwaka 2015, ameachiliwa huru usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa wiki hii.

ISabelle Prime alitekwa nyara akiwa pamoja na mkalimani wake Februari 24 mmwaka 2015 katika mji wa Sanaa, Yémen.
ISabelle Prime alitekwa nyara akiwa pamoja na mkalimani wake Februari 24 mmwaka 2015 katika mji wa Sanaa, Yémen. AFP / MOHAMMED HUWAIS
Matangazo ya kibiashara

Taarifa kutoka Ofisi ya rais wa Ufaransa, Elysee, ambayo imetoa taarifa hiyo, imesema kuwa mateka huyo kwa sasa yuko mikononi mwa Idara za usalama za Udfaransa, na anatazamiwa kuwasili nchini katika mji wa Paris, nchini Ufaransa, mchana wa leo ijumaa Agosti 7.

" Raia mwenzetu Isabelle Prime ameachiliwa huru usiku wa kuamkia leo Ijumaa ", tangazo la Ofisi ya rais limearifu, na kutolewa usiku wa Alhamisi kuamkia leo Ijumaa.

" Ufaransa imefanya kila jitihada ili kufikia matokeo haya mazuri . Isabelle Prime kwa sasa yuko chini ya ulinzi wa Idara za usalama za Ufaransa. Na anatazamiwa kuwasili nchini mwetu katika masaa yajayo ", taarifa hiyo ya Elysee imeeleza, bila hata hivyo kueleza mazingira ya kuachiwa kwake.

Rais wa Ufaransa François Hollande "ameelezea shukurani zake kwa wale wote ambao walichangia ili kufikia suluhisho hilo, ikiwa ni pamoja na Sultani Qaboos Bin Said, mfalme wa Oman".

François Hollande amesema " anachangia furaha na familia ya Isabelle ambayo haikukata tamaa na kuonyesha ujasiri na jukumu kubwa katika kipindi chote hicho cha muda mrefu, wakisubiri hatma ya ndugu yao", kwa mujibu wa chanzo hicho.

Isabelle Prime, aliwasili nchini Yemen mwaka 2013, alifanya kazi katika kampuni ya Ayala Consulting. Alitekwa nyara akiwa pamoja na mkalimani wake, raia wa Yemen Chérine Makkaoui, Februari 24 mwaka huu katika mji wa Sanaa na watu waliojifananisha na askari polisi wakati ambapo walikua wakielekea kazini.

Chérine Makkaoui aliachiliwa huru Machi 10 katika mji wa Aden, kusini mwa Yemen. Baada Baada ya kutekwa nyara kwa raia huyo wa Ufaransa, rais Hollande alidai kuachiliwa kwa mateka huyo " bila kuchelewa ". Chérine Makkaoui mwenye umri wa miaka 30 na ni mwenye asili ya magharibi ya Ufaransa. Mwajiri wake, Francisco Ayala, amesema kuwa Chérine Makkaoui atawasili mjini Paris leo Ijumaa mchana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.