Pata taarifa kuu
UFARANSA-QATAR-SAUDI ARABIA-DIPLOMASIA

François Hollande ziarani Qatar

Rais wa Ufaransa François Hollande amewasili Qatar, Jumatatu Mei 4, ambapo atahuzuria sherehe za kutiwa saini mkataba wa mauzo ya ndege 24 za kivita aina ya Rafale.

François Hollande zirani Doha, Qatar, Juni mwaka 2013.
François Hollande zirani Doha, Qatar, Juni mwaka 2013. REUTERS/Fadi Al-Assaad
Matangazo ya kibiashara

Hollande baadae atajielekeza nchini Saudi Arabia, ambapo atazungumzia na mfalme wa nchi hiyo suala la vita nchini Yemen, Iraq na Syria.

Lakini pia mpango wa Nyuklia wa Iran, ambao unazitia wasiwasi tawala za kifalme za Kisuni za nchi za Ghuba.

François Hollande atapokelewa mjini Doha Jumatatu wiki hii na Amir wa Qatar. Viongozi hao wawili watakuwa na mkutano baina yao kabla ya sherehe rasmi ya kutia saini ya mauzo ya ndege 24 za kivita aina ya Rafale. Ndege ambazo ziliuzwa na Ufaransa kwa Qatar, kiasi cha euro zaidi ya bilioni 6.

Mkataba ambao unathibitisha kupaa hewani kwa ndege ya Ufaransa ambayo tayari imenunuliwa na Misri pamoja na India mwaka huu.

Mwezi Februari mwaka huu, Ufaransa iliiuzia Misri ndege 24 za kivita aina ya Rafale kwa euro bilioni 5.2 ikiwa ni pamoja na vifaa vya ndege hizo.

Baada ya hatua hiyo ya kwanza ya kidiplomasia na biashara, François Hollande anasubiriwa Jumatatu jioni wiki hii nchini Saudi Arabia. Ziara ambayo ni muhimu katika nchi ambapo Mfalme wa nchi hiyo amefanya mageuzi katika utawala wake, wakati ambapo Saudi Arabia na washirika wake kutoka Warabuni wameendelea na mashambulizi dhidi ya waasi wa Huthi nchini Yemen, nchi jirani ya Saudi Arabia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.