Pata taarifa kuu
UFARANSA-RSF-Wanahabari-Tuzo-Usalama

Wanahabari waliouawa watunukiwa tuzo

Camille Lepage, Ghislaine Dupont, Claude Verlon, Anja Niedringhaus, Sardar Ahmad pamoja na James Foley, ni waandishi wa habari waliouawa wakiwa katika shughuli zao za kikazi, hususan kuelezea yanayojiri katika mataifa yanayo kabiliwa na machafuko duniani.

Mnara wa ukumbusho wa wanahabari waliouawa wakiwa katika kazi yao ya uandishi, mjini Bayeux.
Mnara wa ukumbusho wa wanahabari waliouawa wakiwa katika kazi yao ya uandishi, mjini Bayeux. RFI
Matangazo ya kibiashara

Waandishi hao wa habari ambao waliuawa wakiwa ni mashuja katika kazi yao wametunukiwa Alhamisi wiki hii Oktoba 9 tuzo ya Bayeux-Calvados ikiwa ni pamoja na mnara uliyojengwa katika mji wa Bayeux kwa niaba ya waandishi wa habari waliouawa katika miaka ya 2013- 2014.

Ghislanie Dupont na Claude Verlon waliuawa katika mji wa Kidal nchini Mali Novemba 2 mwaka 2013.

Mwaka 2013, ilikua mwaka wa majonzi na msukosuko kwa jamii ya wanahabari duniani kufuatia vifo vya wanahabari ambao waliuawa wakiwa katika kazi yao ya kutafuta habari na kueleza kwa kina kinachoendelea katika mataifa yanaokabiliwa na machafuko aidha migogoro ya wenyewe kwa wenyewe.

Wanahabari 71 waliuawa katika mwaka 2013 pekee, huku 51 wakiwa wameuawa tangu mwanzoni mwa mwaka 2014 wakati ambapo mwaka wenyewe haujafikia tamati.

Kiongozi wa shirika la wanahabari wasio na mipaka RSF, Christophe Deloire, amesema ana imani kuwa mnara huo wa ukumbusho wa wanahabari waliouawa wakiwa katika kazi yao, ndio wa mwisho kujengwa.

“ Nina imani kwamba hakutokuweko tena na mwaandishi wa habari ambaye atauawa akiwa katika kazi yake, baada ya hawa ambao utaendelea kukumbuka”, amesema Deloire mbele ya mnara wa ukumbusho wa wahanga katika taaaluma ya uandishi mjini Bayeux Oktoba 9 mwaka 2014.

Majina ya wanahabari waliouawa katika miaka 2013-2014 yamewekwa kwenye mnra huu uliyojengwa mjini Bayeux.
Majina ya wanahabari waliouawa katika miaka 2013-2014 yamewekwa kwenye mnra huu uliyojengwa mjini Bayeux. RFI

Majina ya Camille Lepage, Ghislaine Dupont, Claude Verlon, Anja Niedringhaus, Sardar Ahmad pamoja na James Foley yameongezwa kwenye orodha ya wanahabari waliouawa wakiwa katika kazi yao. 

Familia, jamaa na marafiki wa wahanga hao wamehudhuria katika sherehe hizo, huku wakifumbatiana kama ishara ya kuwakumbuka ndugu zao.

Apolline, msichana wa Claude Verlon, mbele ya eneo kulikoandikwa jina la baba yakee. Jamaa na marafiki wa Ghislaine Dupont walihudhuria pia sherehe hizo.
Apolline, msichana wa Claude Verlon, mbele ya eneo kulikoandikwa jina la baba yakee. Jamaa na marafiki wa Ghislaine Dupont walihudhuria pia sherehe hizo. RFI

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.