Pata taarifa kuu

Uhispania: Msamaha kwa watu wanaotaka kujitenga wa Catalonia walalamikiwa

Makumi ya maelfu ya Wahispania wameandamana mjini Madrid, Plaza de España, kupinga sheria inayotoa msamaha kwa watu wanaotaka kujitenga wa Catalonia walioshitakiwa kwa jaribio la kujitenga mwaka 2017. Maandamano hayo, yaliyoitishwa na Chama cha Popular Party (PP, cha mrengo wa kulia) yamewaleta pamoja watu 45,000, kulingana na halmashauri ya mkoa wa Madrid. Sheria ya baadaye, inayolingana na kuchaguliwa tena kwa Waziri Mkuu Pedro Sánchez, itawasilishwa kwa Congress mnamo Jumanne Januari 30.

Makumi ya maelfu ya Wahispania walikusanyika katikati ya jiji la Madrid kupinga sheria ya msamaha kwa watu wanaotaka kujitenga wa Catalonia walioshtakiwa kwa jaribio la kujitenga la 2017 lililotibuliwa, Januari 28, 2024.
Makumi ya maelfu ya Wahispania walikusanyika katikati ya jiji la Madrid kupinga sheria ya msamaha kwa watu wanaotaka kujitenga wa Catalonia walioshtakiwa kwa jaribio la kujitenga la 2017 lililotibuliwa, Januari 28, 2024. AFP - OSCAR DEL POZO
Matangazo ya kibiashara

 

"Kati ya msamaha na demokrasia, lazima tuchague, na tunachagua demokrasia." Hii ni mojawapo ya kauli mbiu kuu ambazo zimesikika katika eneo la Plaza de España huko Madrid, anasema mwandishi wa RFI huko Madrid, François Musseau.

Wengi wamepeperusha bendera za zenye damu na dhahabu na kudai kuwa msamaha kwa viongozi wanaotaka kujitenga wa Catalonia ni usaliti kwa upande wa mwanasoshalisti Pedro Sanchez, aliye madarakani. Kwa hakika tulimwona Alberto Nuñez Feijoo, kiongozi wa mreno wa kulia wa kihafidhina, ambaye kwake, "serikali ya Sanchez ni kikundi cha watu wenye maslahi mbalimbali, ambayo yataanguka mapema kuliko baadaye". Kabla ya kuongeza: "tunakwenda kuokoa nchi hii kwa njia ya kidemokrasia".

Zaidi ya yote, tulikuwa na hisia ya kuhudhuria mkutano wa kabla ya uchaguzi kwa ajili ya uchaguzi wa Ulaya Juni ijayo, ambapo mrengo wa kulia natarajia kupata mtunda mazuri. Machoni mwa waandamanaji, Pedro Sanchez, aliyewakilishwa na mwanasesere mkubwa anayening'inia miguuni mwake, anadhamiria kuiuza Uhispania kwa watu wanaotaka kujitenga kwa Basque na Catalonia . Kwa maandamano haya, mrengo wa kulia unashambulia kifua. Lakini kwa sasa, unapambana na mamlaka ambayo, Jumanne hii, Januari 30, inapaswa kupitisha sheria yake maarufu ya msamaha.

Pedro Sánchez, kitendo cha kusawazisha cha siasa za Uhispania

Uwezekano wa kurejea Uhispania kwa Carles Puigdemont, mkuu wa zamani wa serikali katika eneo la Catalan wakati wa jaribio la kujitenga kwa eneo hili mwaka 2017 na ambaye anaishi Ubelgiji kwa miaka saba, kunawatia wasiwasi baadhi ya waandamanaji. Kwa wengine, ni "tusi". Wengine wanasikitishwa kwamba Carles Puigdemont anaweza kuepuka kufuatiliwa na mahakama, "Sina neno, ni mtu ambaye amehukumiwa".

Itakapopigiwa kura na kutangazwa, pengine sio kwa miezi kadhaa, sheria ya msamaha itaruhusu, ndani ya miezi miwili, kuondolewa kwa kesi dhidi ya mamia ya wanaharakati na viongozi wa uhuru walioshtakiwa kwa jukumu lao katika jaribio la kujitenga kuanzia 2017.

Sheria hii iliyoahidiwa na Pedro Sanchez ilimruhusu kuteuliwa tena kama mkuu wa serikali katikati ya Novemba 2023 kwa muhula mpya wa miaka minne kutokana na kura za wabunge wa vyama viwili vilivyojitenga vya Catalonia, ambao waliweka masharti yao msaada.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.