Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Serbia: Rais Aleksandar Vucic anadai ushindi wa chama chake katika uchaguzi wa wabunge

Rais wa Serbia Aleksandar Vucic amedai Jumapili usiku ushindi wa chama chake cha SNS katika uchaguzi wa wabunge, ambapo ambaye anasema ameshinda kwa angalau viti 127 kati ya 250 vya Bunge.

Rais wa Serbia Aleksandar Vucic mnamo Desemba 17 huko Belgrade.
Rais wa Serbia Aleksandar Vucic mnamo Desemba 17 huko Belgrade. AP - Darko Vojinovic
Matangazo ya kibiashara

"Tutakuwa na wingi kamili wa viti katika Bunge kwa kupata viti 127," ametangaza Aleksandar Vucic akijiamini katika mkutano na waandishi wa habari, kulingana na 76% ya kura zilizohesabiwa. Wakati wa uchaguzi wa wabunge ulilopita, SNS ilikuwa na viti 120.

Akiwa kila mahali kwenye vyombo vya habari, rais aliangaziwa, akifanya uchaguzi huu wa wabunge na serikali za mitaa kuwa kura ya maoni juu ya yake. "Kazi yangu ilikuwa kufanya kila kitu katika uwezo wangu ili kupata wingi kamili wa kura katika Bunge," ametangaza Jumapili usiku, akisema "anajivunia" kampeni iliyofanywa.

Matokeo rasmi hayatarajiwi kabla ya Jumatatu jioni, lakini upinzani, ulioungana chini ya kauli "Serbia dhidi ya vurugu", ulipata 23.5% ya kura. Muungano huu, ulioanzishwa kutokana na maandamano makubwa ambayo yalitikisa nchi mwezi Mei, baada ya vifo vya watu 19 kwa matukio mawili ya kupigwa risasi - ikiwa ni pamoja na moja katika shule ya msingi - ulikuwa bado haujazungumza hadi Jumapili usiku. Muungano huo umeendelea kushutumu kampeni ya upendeleo, iliyochafuliwa na udanganyifu.

Upinzani walaani makosa

Kiongozi wake, Radomir Lazovic, alizungumzia dosari siku ya Jumapili asubuhi - akithibitisha kwamba labda ulikuwa "mchakato mchafu zaidi wa uchaguzi", akimaanisha "kununua kura, saini za uwongo..." Upinzani pia ulidai kuwa mabasi yote yalifika Belgrade huku yakiwabeba watu wasio wakazi wa mji huo kwa minajili ya kupiga kura.

"Wasiwasi mkubwa unasababishwa na idadi kubwa ya wapiga kura walioletwa Belgrade kutoka maeneo mengine," kimesema Kituo cha Utafiti, Uwazi na Uwajibikaji (CRTA), ambacho timu yake ya waangalizi imedai kushambuliwa huko Odzaci (kaskazini-mashariki); "baada ya kurekodi kesi ya rushwa katika uchaguzi, ambapo kura nyingi zilipelekwa katika ofisi za vyama vya siasa."

Shutuma ambazo Waziri Mkuu Ana Brnabic alifutilia mbali wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jumapili jioni. Katika zoezi ambalo pia ni la kawaida kwa rais, ameushutumu upinzani kwa kutaka kuzua fujo kwa madai ya uwongo.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.