Pata taarifa kuu

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, awasili nchini Jordan

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, amewasili nchini Jordan ambako atakutana kwa mazungumzo na mfalme Abdulah wapili, ziara inayolenga kutafuta uungwaji mkono wa juhudi za Ufaransa katika kupata suluhu ya mzozo wa ene la mashariki ya kati.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akizungumza wakati wa mkutano na waalimu kwenye ikulu  ya Elysee  huko Paris.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akizungumza wakati wa mkutano na waalimu kwenye ikulu ya Elysee huko Paris. AP - Christophe Petit Tesson
Matangazo ya kibiashara

Macron anawasili Jordan akitokea nchini Israel na Jerusalem magharibi, ambapo kwa nyakati tofauti alikutana na waziri mkuu Benjamin Netanyahu na rais wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas.

Akiwa Israel, Macron aliahidi nchi yake kuendelea kusimama na Israel, akiitaka nchi hiyo kuheshimu sheria za kimataifa inapotekeleza operesheni zake kwenye ukanda wa Gaza, ambapo pia ametaka kundi la Hamas kukabiliwa kama ilivyo kwa Islamic State.

Aidha katika mazungumzo yake na rais Abbas, macron, amesema nchi yake itahakikisha haki za Wapalestina zinalindwa, akiahidi kushinikiza kupelekwa kwa misaada zaidi.

Kutoka Jordan, rais Macron ataelekea Misri kukutana na rais Abdel Sisi, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kutafuta uungwaji mkono baada ya ziara ya rais wa Marekani na Ujerumani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.