Pata taarifa kuu

Kiongozi wa Uturuki asema Hamas ni 'kundi la ukombozi'

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema Hamas ni kundi la ukombozi linaloendesha vita kulinda ardhi yake.


Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akitoa hotuba katika ikulu ya rais, mjini Ankara, Uturuki, Jumapili, Mei 28, 2023.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akitoa hotuba katika ikulu ya rais, mjini Ankara, Uturuki, Jumapili, Mei 28, 2023. AP - Ali Unal
Matangazo ya kibiashara

Hamas - au katika hali nyingine tawi lake la kijeshi - limetajwa kuwa kundi la kigaidi na Israel, Marekani, EU na Uingereza, pamoja na mataifa mengine yenye nguvu.

Zaidi ya watu 1,400 waliuawa katika mashambulizi ya Hamas dhidi ya Israel tarehe 7 Oktoba.

Katika hotuba yake katika bunge la Uturuki, Erdogan alisema alikuwa akighairi mipango ya awali ya kuzuru Israel.

Alisema amewahi kumsalimia kwa mkono Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, lakini ametumia vibaya nia njema ya Uturuki.

Viongozi hao wawili walikutana mwezi uliopita katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa mjini New York - katika kile kilichoonekana wakati huo kama ishara nyingine muhimu ya kuboreka kwa uhusiano kati ya nchi zao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.