Pata taarifa kuu

Indo-Pacific: Nchi 13 zakusanyika kwa mazoezi ya kijeshi kwenye pwani ya Australia

Mazoezi ya kijeshi ya kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa, yakihusisha zaidi ya wanajeshi 30,000 kutoka nchi kumi na tatu, ikiwa ni pamoja na Marekani, Australia na Ufaransa, yalianza siku mbili zilizopita kwenye pwani ya Australia. Operesheni inayoitwa "Talisman Sabre", ambayo ni yenye manufaa makubwa. Kwa hivyo, meli ya kijasusi ya Kichina ilionekana tangu kuanza kwa mazoezi haya kwenye bahari kuu.

Jaribio la kurusha kombora kama sehemu ya Operesheni ya Talisman Sabre nchini Australia.
Jaribio la kurusha kombora kama sehemu ya Operesheni ya Talisman Sabre nchini Australia. AFP - ANDREW LEESON
Matangazo ya kibiashara

Kuonyesha misuli na uwezo wa kuingilia kati pamoja katika operesheni sawa. Hili ndilo lengo la operesheni hii ya "Talisman Sabre", ambayo inaleta pamoja wanajeshi 30,000 kutoka nchi kumi na tatu. Wanajeshi wa Japan, kwa mara ya kwanza, walifanya mazoezi ya kurusha makombora katika pwani ya mashariki ya Australia wakati wa operesheni hii.

Mazoezi haya yanalenga kuimarisha ushirikiano kati ya majeshi ya nchi yanayoendeshwa na nia sawa: "Kulinda eneo salama, linalostahimili na lenye mafanikio la Indo-Pacific. Ni wazi kwamba ni suala la kuionyesha China kwamba nchi za Magharibi na washirika wao hazikusudii kuiruhusu kupanua wigo wake wa ushawishi katika eneo hilo, anaeleza mwandishi wetu wa habari huko Melbourne, Grégory Plese. Haishangazi, Beijing haishiriki katika operesheni hii.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.