Pata taarifa kuu

Ufaransa yawarejesha nyumbani wanawake 10 na watoto 25 kutoka kambi za wanajihadi Syria

Paris imewarejesha nyumbani leo Jumanne Julai 4 wanawake kumi na watoto ishirini na watano waliokuwa wamezuiliwa katika kambi za wapiganaji wa kijihadi kaskazini mashariki mwa Syria, Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa imetangaza. Hii ni operesheni ya nne ya pamoja katika mwaka mmoja.

Raia hao wa Ufaransa wanaishi pamoja na wanawake wengine wa mataifa mbalimbali katika kambi za Al-Hol na Roj (pichani) zinazodhibitiwa na Wakurdi, ambako ghasia hutokea mara kwa mara na ambapo kunyimwa haki kumekithiri.
Raia hao wa Ufaransa wanaishi pamoja na wanawake wengine wa mataifa mbalimbali katika kambi za Al-Hol na Roj (pichani) zinazodhibitiwa na Wakurdi, ambako ghasia hutokea mara kwa mara na ambapo kunyimwa haki kumekithiri. AP - Maya Alleruzzo
Matangazo ya kibiashara

Wanawake wa Ufaransa waliorudishwa nyumnani nchini Ufaransa walikuwa wamekwenda kwa hiari katika maeneo yanayodhibitiwa na makundi ya jihadi katika eneo linalounganisha Iraq na Syria. Kisha, walikamatwa wakati wa utawala wa kundi la Islamic State ulipoanguka mwaka wa 2019. Wnawake hao wamekabidhiwa kwa "mamlaka zinazofaa za mahakama", inabainisha Quai d'Orsay katika taarifa kwa vyombo vya habari. "Watoto wadogo wamekabidhiwa kwa idara zinazohusika na ustawi wa watoto" na watakuwa chini ya ufuatiliaji wa matibabu na kijamii.

Siku ya Jumanne, "Ufaransa imeshukuru utawala wa eneo la kaskazini mashariki mwa Syria kwa ushirikiano wake, ambao ulifanikisha operesheni hii". Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Kitaifa wa Kupambana na Ugaidi imesema katika taarifa yake kwamba kati ya wanawake hao kumi, wenye umri wa miaka 23 hadi 40, saba waliwekwa chini ya ulinzi wa polisi mara moja katika kutekeleza hati ya upekuzi na kwamba wengine watatu, wanalengwa na hati ya upekuzi. walipelekwa mchana kwa hakimu wa uchunguzi kwa nia ya kufunguliwa mashitaka. Aidha, miongoni mwa watoto hao, msichana mwenye umri wa miaka 17 pia aliwekwa chini ya ulinzi wa polisi.

Mtu mzima yeyote ambaye amejiunga na eneo linalounganisha Iraq-Syria na ambaye atasalia hapo atakabiliwa na mashtaka ya kisheria. Katika majira ya joto ya mwaka 2022, Ufaransa ilikomesha sera ya "kesi kwa kesi", ambayo iliifanya kulaaniwa na mashirika ya kimataifa na lawama.

Kwa jumla, wanawake 16 na watoto 35 walirudishwa Ufaransa wakati wa operesheni ya kwanza ya pamoja mwaka mmoja uliopita, ikifuatiwa mwezi Oktoba na kurudi kwa wanawake 15 na watoto 40. Mwezi Januari, Ufaransa ilitangaza kuwarejesha nyumbani wanawake 15 na watoto 32, siku chache baada ya kulaaniwa na Kamati ya Umoja wa Mataifa dhidi ya Mateso.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.