Pata taarifa kuu
UFARANSA-SYRIA-IS-USALAMA

Maafisa muhimu wa wanajihadi kutoka Ufaransa wakamatwa Syria

Maafisa kadhaa wa kundi la Islamic State ikiwa ni pamoja na Thomas Barnouin wanashikiliwa nchini Syria. Thomas Barnouin ambaye ni miongoni mwa wanajihadi kutoka Ufaransa waliokua wakitafutwa alikamatwa tarehe 17 Desemba na wapiganaji wa Kikurdi nchini Syria.

Wanajihadi watatu kutoka Ufaransa washikiliwa Syria na vikosi vya Kikurdi. Hii hapa ni bendera ya kundi la Islamic State.
Wanajihadi watatu kutoka Ufaransa washikiliwa Syria na vikosi vya Kikurdi. Hii hapa ni bendera ya kundi la Islamic State. DELIL SOULEIMAN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Taarifa ya kukamatwa kwake ilitolewa siku ya Jumatano Desemba 27.

Thomas Barnouin, mwenye umri wa miaka 36, mkazi wa Albi, mji ulio kusini magharibi mwa Ufaransa ni miongoni mwa maafisa wakuu wa kundi la Islamic State, kwa mujibu wa idara za usalama za Ufaransa.

Katikati ya mwaka 2000, Thomas Barnouin alikuatana na Mohamed Merah, ambaye aliua mwezi Machi mwaka 2012 watu saba mjini Toulouse na Montauban, lakini pia ndugu wa Clain, ambapo sauti zao zilijulikana katika madai kupitia ujumbe wa sauti ya kundi la Islamic State kuhusu mashambulizi ya Novemba 2015 mjini Paris, nchini Ufaransa.

Thomas Barnouin ambaye alikamatwa kwa mara ya kwanza nchini Syria mwaka 2006 na kisha kufukuzwa nchini Ufaransa, alihukumiwa mwaka 2009 hadi miaka mitano gerezani. Mwaka 2014, licha ya kufuatiliwa na polisi, Thomas Barnouin aliweza kusafiri kwenda Syria akiongozana na Waislam wengine wenye msimamo mkali kutoka eneo la Midi-Pyrénées.

Thomas Barnouin na wanajihadi wengine wawili wa Ufaransa kwa sasa wanashikiliwa na vikosi vya Kikurdi. Wanakabiliwa na adhabu ya kifo kwa kushirikiana na kundi la Islamic State.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.