Pata taarifa kuu

Nyambizi iliyotoweka: Zimesalia saa 20 tu kuwapata manusura katika meli ya 'Titan'

Walinzi wa Pwani wa Marekani wamesema siku ya Jumatano kuwa bado hawajapata nyambizi iliyotoweka karibu na mabaki ya meli kubwa "Titanic", huku uwezo wa oksijeni kwenye meli hiyo ya watalii 'Titan' iliyotoweka, ukipungua.

Askari wa kikosi cha walinzi wa Pwani wa Marekani (USCG) Kapteni Jamie Frederick akizungumza na waandishi wa habari kuhusu jitihada za kutafuta meli ndogo ya Titan iliyozama chini ya maji ambayo ilitoweka karibu na mabaki ya meli kubwa ya Titanic, katika Kituo cha Walinzi wa Pwani huko Boston, Massachusetts, Juni 21, 2023.
Askari wa kikosi cha walinzi wa Pwani wa Marekani (USCG) Kapteni Jamie Frederick akizungumza na waandishi wa habari kuhusu jitihada za kutafuta meli ndogo ya Titan iliyozama chini ya maji ambayo ilitoweka karibu na mabaki ya meli kubwa ya Titanic, katika Kituo cha Walinzi wa Pwani huko Boston, Massachusetts, Juni 21, 2023. AFP - JOSEPH PREZIOSO
Matangazo ya kibiashara

Zoezi la kutafuta meli hiyo ndogo bado linaendelea, Jumatano hii, Juni 21, kujaribu kuipata nyambizi hiyo iliyotoweka Jumapili, Juni 18, kwenye Bahari ya Atlantiki. Baada ya siku tatu za ukimya, "kelele" za kawaida, zinazorudia "kila dakika 30", zilinaswa Jumatano hii chini ya maji na Walinzi wa Pwani ya Marekani, kwa kutumia ndege za P-3 za Canada zilizotumwa kwenye eneo la tukio.

"Hatujui" asili ya sauti zilizonaswa baharini wakati wa zoezi linaloendeshwa chini ya maji kuwatafuta watu watano waliokuwa ndani ya meli hii ya kitalii, waliokuwa wamekwenda kuchunguza ajali ya meli ya Titanic, walinzi wa Pwani wa Marekani wamesema kwenye mkutano Jumatano. “Siwezi kuwambia hizo kelele ni za nini. Ninachoweza kuwaambia, na hili ndilo jambo muhimu zaidi, ni kwamba tunatafuta mahali ambapo sauti" zilinaswa, amesema nahodha Jamie Frederick, na kuongeza kwamba lazima "tubaki na matumaini ya kuwapata wakiwa hai", wakati hifadhi ya oksijeni inapaswa kuisha siku ya Alhamisi katika chombo hiki kilichotoweka.

Meli hiyo iitwayo Titan ilienda kuchunguza vilindi karibu na mabaki ya meli kubwa ya Titanic - iliyoko mita 4000 kwenda chini - ikiwa na watu watano, akiwemo mfanyabiashara Hamish Harding na mpiga mbizi wa zamani wa Ufaransa Paul- Henry Nargeolet. Chombo hicho hakijatoa dalili zozote za watu kuwa hai tangu saa tatu na dakika 13 usiku siku ya Jumapili, karibu saa mbili baada ya kuingia majini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.