Pata taarifa kuu
USALAMA- MAJINI

Utafutaji wa nyambizi ya 'Titan': Ufaransa yatuma 'Atalante'

Ufaransa inatuma meli kubwa na roboti yake ya hali ya juu kujaribu kutafuta nyambizi ndogo ya watalii ya Titan, ambayo haijapatikana katika Bahari ya Atlantiki tangu Jumapili Juni 19. Watu watano waliokuwa kwenye nyambizi hiyo walikuwa wamekwenda kuchunguza mabaki ya meli kubwa ya Titanic, ambayo yako karibu mita 3,800 kwenda chini, kutoka Canada na Marekani, tangu mwaka 1912. Ndege, meli zinaendelea na zoezi hilo, katika mazingira magumu sana.

Nyambizi ya kitalii ya 'Titan', ambayo ilitoweka siku ya Jumapili ilipokuwa kwenye matembezi kuhusu ajali ya "Titanic", katika Bahari ya Atlantiki.
Nyambizi ya kitalii ya 'Titan', ambayo ilitoweka siku ya Jumapili ilipokuwa kwenye matembezi kuhusu ajali ya "Titanic", katika Bahari ya Atlantiki. AP
Matangazo ya kibiashara

Taasisi ya Utafiti ya Ufaransa ya Unyonyaji wa Bahari (IFREMER) inatoa wito kwa Atalante, ambayo imeelekezwa kutoka kwa misheni yake ya sasa kufikia eneo hilo, katika Bahari ya Atlantiki ya Kaskazini, ambapo Titan ilipotea. Hervé Berville, waziri mwenye dhamana ya Bahari, ndiye ambaye ametangaza.

Meli hii ya Ufaransa ina roboti inayoendeshwa kwa mbali chini ya maji ya kina kirefu, Victor 6000. "Kifaa kitaendelea kwa kushirikiana na kituo cha uratibu wa NATO na tunawasiliana na mamlaka ya Marekani", amesema Bw. Berville.

Muungano wa Atlantic umeonyesha kuwa vifaa vyake vya uokoaji haviwezi kwenda chini zaidi ya mita 2,000, lakini kwamba inaweza kufanya utaalamu wake na uwezo wa uchambuzi kupatikana, kama anavyoripoti mwandishi wetu wa Washington, Guillaume Naudin.

Vifaa vya Ufaransa vinatarajiwa katika eneo hilo siku ya Jumatano karibu saa mbili kamili usiku. Waendeshaji wa roboti pia wako njiani, waliondoka Toulon na watafika Newfoundland nchini Canada Jumatano asubuhi, saa za Ufaransa.

Hadi wakati huo, utafutaji unaendelea. Manowari ya Titan ina urefu wa mita 6.5 na urefu wa mita 2.5 kwenda juu. Ni kana kwamba huduma za uokoaji zilikuwa zinatafuta basi dogo katikati ya bahari, katika eneo la 13,000 km², sawa na nchi yenye ukubwa wa Montenegro.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.