Pata taarifa kuu

Vurugu Kosovo: Emmanuel Macron ashutumu 'wajibu wa mamlaka ya Kosovo'

Mvutano unaongezeka kati ya Kosovo na jamii ya Waserbia walio wachache nchini humo. Kutoka Bratislava, Emmanuel Macron ameshutumu "wajibu wa mamlaka ya Kosovo".

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akizungumza wakati wa kongamano la usalama la eneo la Globsec huko Bratislava, Slovakia, Mei 31, 2023.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akizungumza wakati wa kongamano la usalama la eneo la Globsec huko Bratislava, Slovakia, Mei 31, 2023. AFP - MICHAL CIZEK
Matangazo ya kibiashara

Katika mvutano huo ambao kwa sasa unaohusisha Kosovo na Waserbia walio wachache, Emmanuel Macron ameamua kuonyesha msimamo wake. Katika ziara ya kiserikali nchini Slovakia siku ya Jumatano, Rais wa Jamhuri amelaani vikali tabia ya mamlaka ya Kosovo, inayowajibika katika mgogoro wa wazi kati ya wengi wa Albania na wachache wa Serbia.

"Ni wazi kabisa, kuna jukumu kwa upande wa mamlaka ya Kosovo katika hali ya sasa na kushindwa kuheshimu makubaliano ambayo hata hivyo yalikuwa muhimu na ambayo yalitiwa saini wiki chache zilizopita," Rais Macron amesema katika mkutano na waandishi wa habari huko Bratislava. Emmanuel Macron amekosoa mamlaka ya nchi kwa kuingiza mameya wa Albania katika miji kadhaa, baada ya uchaguzi kususiwa na Waserbia na viwango vya ushiriki visivyozidi 3.5%. "Tulifahamisha wazi kwa mamlaka ya Kosovo kwamba lilikuwa kosa kuendelea na uchaguzi huu", ameongeza rais wa Ufaransa.

Jeshi la Serbia lawekwa karibu na mpaka wa Kosovo

Uchaguzi wa serikali za mitaa umechochea uhasama huo kati ya mamlaka ya Kosovo na Waserbia kaskazini mwa nchi, ambao wanasalia watiifu kwa Belgrade na hawatambui mamlaka ya Pristina. Mapigano makali kati ya Waserbia na kikosi cha KFOR siku ya Jumatatu yalisababisha wanajeshi 30 wa NATO kujeruhiwa.

Kwa upande wake Rais wa Serbia Aleksandar Vučić ametangaza kupeleka jeshi lake karibu na mpaka wa Kosovo. Katika jaribio la kutuliza mvutano, Emmanuel Macron ametangaza nia yake ya "kuwaona rais wa Kosovo na rais wa Serbia pamoja" siku ya Alhamisi, kando ya mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Kisiasa ya Ulaya huko Moldova.

Mnamo 1999, Kosovo, ikiungwa mkono na muungano wa Magharibi ikijumuisha Ufaransa, ilipata uhuru wake baada ya vita dhidi ya Serbia. Mzozo huo uligharimu maisha ya watu zaidi ya 13,000, wengi wao wakiwa raia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.