Pata taarifa kuu

Bunge la Ureno lahalalisha matumizi ya dawa aina ya Euthanasia

Ureno hii leo imepitisha sheria ya kuhalalisha matumizi ya dawa ya euthanasia kwa watu walio katika mateso makubwa na magonjwa yasiyotibika, wakijiunga na nchi chache tu ulimwenguni.

Ureno imehalalisha matumizi ya  euthanasia
Ureno imehalalisha matumizi ya euthanasia GETTY IMAGES NORTH AMERICA/AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Upinzani mkali  kuhusu matumizi ya dawa hiyo umeshuhudiwa kutoka kwa Rais wa kihafidhina Marcelo Rebelo de Sousa.Baadhi ya masharti ya dawa hio ni kuwa walioko chini ya umri wa miaka 18 hawataruhusiwa kuitumia na hata walioko na umri wa zaidi ya miaka 18 watatumia tuu iwapo wapo kwenye hali mahututi.

Sheria hiyo itatumika tu kwa raia na wakaazi halali na sio kwa wageni wanaokuja nchini kutafuta usaidizi wa kujiua.

Mswada wa euthanasia uliidhinishwa na bunge mara nne katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita lakini ulirejeshwa kila mara kwa ajili ya mapitio ya katiba kutokana na upinzani kutoka kwa rais.

Toleo mahususi la sheria hiyo lilipitishwa siku ya Ijumaa kwa uungwaji mkono kutoka kwa Wasoshalisti watawala, ambao wanashikilia kura nyingi katika bunge.

"Tunathibitisha sheria ambayo tayari imeidhinishwa mara kadhaa na wengi," Mbunge wa Kisoshalisti Isabel Moreira, mtetezi wa  mpango huo wa kuhalalisha euthanasia.

Rebelo de Sousa alikuwa amepinga miswada ya awali kutokana na "dhana ambazo hazijafafanuliwa kupita kiasi" na baadaye akasema lugha inayotumika kuelezea hali ya wastaafu iliendelea kukinzana na inahitaji kufafanuliwa.

Toleo jipya la sheria sasa linatoa kwamba euthanasia inaidhinishwa tu katika hali ambapo "kujiua kwa msaada wa kimatibabu haiwezekani kutokana na ulemavu wa kimwili wa mgonjwa".

Rebelo de Sousa amewataka wabunge kubainisha ni nani "angethibitisha" ikiwa mgonjwa hakuwa na uwezo wa kusaidiwa kujiua lakini wabunge wakati huu walikataa kurekebisha maandishi.

Maswali yaliyoibuliwa na rais yanaweza kushughulikiwa kupitia utekelezaji wa amri, alisema Catarina Martins, kiongozi wa Kambi ya mrengo mkali wa kushoto.

Rebelo de Sousa mwenyewe alisema uidhinishaji wa sheria hiyo "haukuwa mchezo wa kuigiza" na haukusababisha "matatizo ya kikatiba".

Mjadala kuhusu kufa kwa kusaidiwa na matibabu uko mbali sana nchini Ureno.

"Kupitishwa kwa sheria hii kumekuwa kwa kasi ikilinganishwa na nyingine kubwa

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.