Pata taarifa kuu

Viongozi kutoka Afrika wawasili London kwa sherehe ya kutawazwa kwa Charles III

Nairobi – Viongozi wa Afrika wamewasili London kwa sherehe ya kutawazwa kwa Mfalme Charles itakayofanyika kesho.Wengi wa viongozi hao ni kutoka nchi za Jumuiya ya Madola.

Mfalme Charles wa III atatawazwa kesho ,London
Mfalme Charles wa III atatawazwa kesho ,London REUTERS/Abir Sultan/Pool
Matangazo ya kibiashara

Paul kagame wa Rwanda, Lazarus Chakwera wa Malawi na George Weah wa Liberia ni miongoni mwa viongozi waliowasili Uingereza .

Rais Emmerson Mnangagwa atakuwa kiongozi wa kwanza wa Zimbabwe kuzuru London kwa zaidi ya miongo miwili baada ya Uingereza kuiwekea vikwazo nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.

Bw Mnangagwa alisema "alifurahi" kupokea mwaliko wa kuhudhuria hafla hiyo ya kifalme.

Kufikia sasa hakuna taarifa yoyote iwapo Rais wa Kenya William Ruto atahudhuria sherehe hizo hata baada ya wiki iliyopita kutoa malalamishi kuwa viongozi wa Afrika wanadhulumiwa ifikiapo ni ziara za nje.

Ruto alikuwa akiashiria tukio ambapo marais wa Afrika walipandishwa basi ili kuhudhuria mazishi ya Malkia Elizabeth nchini Uingereza mwaka uliopita.Waziri Mkuu wa Cameroon Joseph Dion Ngute atamwakilisha Rais Paul Biya kwenye hafla hiyo.

Mfalme Charles wa tatu mwenye umri wa miaka 74, alipanda kwenye kiti cha enzi baada ya kifo cha mama yake Malkia Elizabeth II mnamo mwezi Septemba mwaka uliopita na  ndiye mtu mzee zaidi kuwahi kutangazwa kuwa Mfalme nchini Uingereza.

Katika miaka michache iliyopita, hata hivyo, baadhi ya mataifa ya Jumuiya ya Madola yameanza kujadili uhusiano wao na Taji la Uingereza. Kama sehemu ya mchakato huu, Barbados ilifanya uamuzi wa kuwa jamhuri mwishoni mwa 2021, ambayo ilimuondoa marehemu Malkia kama mkuu wa nchi na kumaliza ushawishi wa karne nyingi za Uingereza juu ya kisiwa hicho, ambacho kilikuwa kitovu cha biashara ya utumwa iliyovuka Atlantiki kwa zaidi ya miaka 200.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.