Pata taarifa kuu

Polisi wamkamata mshukiwa wa shambulio la pili la risasi nchini Serbia.

Nairobi – Polisi nchini Serbia wanamshikilia mshukiwa wa mauaji yaliyosababisha vifo vya watu 8 na majeruhi 13 katika shambulio la pili la risasi wiki hii.

Polisi waweka ulinzi mkali baada ya shambulo la risasi nchini serbia
Polisi waweka ulinzi mkali baada ya shambulo la risasi nchini serbia AFP - ANDREJ ISAKOVIC
Matangazo ya kibiashara

Mtu huyo mwenye silaha  aliripotiwa kufyatua risasi moja kwa moja kutoka kwenye gari karibu na kijiji kilichopo km 60 (maili 37) kusini mwa mji wa Belgrade kabla ya kutoweka.

Mapema wiki hii, mvulana mwenye umri wa miaka 13, aliwauwa wanafunzi wanane katika shule iliyopo mjini Belgrade katika tukio baya zaidi la ufyatuaji risasi kuwahi kushuhudiwa nchini Serbia kwa miaka.

Mapema leo , vyombo vya habari vya Serbia vimesema kuwa kikosi maalumu cha polisi kimewasili katika vijiji vya Mladenovac na Dubona, ambako mauaji ya hivi karibuni yalitokea.

Maafisa wa polisi wameonekana kuweka ulinzi katika vituo mbalimbali .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.