EU na Uingereza zakubaliana kuhusu biashara na Ireland Kaskazini
NAIROBI – Uingereza na Umoja wa Ulaya, zimeafikiana kuhusu mkataba mpya wa kushirikiana kibiashara na Ireland Kaskazini.
Imechapishwa:
Cheza - 00:19
Hii imekuja baada ya Uingereza kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya maarufu kama Brexit mwaka 2020.
Waziri Mkuu Rishi Sunak, amesifia maafikiano hayo.
“Makubaliano ya leo yanahakikisha kwamba kuna hali nzuri ya kufanya biashara nchini Uingereza, yanalinda masilahi ya Ireland Kaskazini katika muungano wetu.” amesema Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak
Ireland Kaskazini ni sehemu ya Uingereza, lakini inapakana na Ireland ambayo ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya, hali ambayo ilikuwa inazua sintofahamu kuhusu ushirikiano wa kibiashara.