Pata taarifa kuu

Uhalifu dhidi ya watoto Kanisani: Waathiriwa 4815 warekodiwa nchini Ureno tangu 1950

Takriban watoto 4,815 wameathiriwa na unyanyasaji wa kijinsia katika Kanisa Katoliki la Ureno tangu mwaka 1950, kulingana na hitimisho zilizosilishwa Jumatatu, Februari 13, na tume huru iliyosikiliza zaidi ya mashuhuda 500 wakati wa kazi yake iliyodumu mwaka mmoja.

Kanisa likionekana kwenye vio kwenye dirisha la duka huko Lisbon.
Kanisa likionekana kwenye vio kwenye dirisha la duka huko Lisbon. AP - Armando Franca
Matangazo ya kibiashara

"Shuhuda hizi huturuhusu kufikia mtandao mkubwa zaidi wa waathiriwa, unaohesabiwa kwa idadi ya chini ya waathiriwa 4,815," mratibu wa tume hii ya wataalam, Daktari wa magonjwa ya akili ya watoto Pedro Strecht, wakati wa uwasilishaji wa ripoti yao. Idadi kubwa ya uhalifu ulioshutumiwa tayari imerekodiwa, lakini ushahidi ishirini na tano umetumwa kwa mwendesha mashtaka wa umma, amebaini.

Mwishoni mwa mwaka 2021, viongozi wa Kanisa la Ureno walimwagiza Pedro Strecht kuunda timu ya kuchukua hatua ya matukio ya uhalifu wa watoto miongoni mwao. Mkuu wa kamati wa maaskofu wa Ureno, askofu wa Leiria-Fatima José Ornelas, anatarajia kuzungumzia hali hiyo leo Alaasiri.

Maaskofu wa Ureno pia wanapanga kukutana mapema mwezi Machi ili kupata hitimisho kutoka kwa ripoti hiyo huru na "kutokomeza kadiri iwezekanavyo janga hili kutoka kwa maisha ya Kanisa", katibu wa kamati ya maaskofu, Padre Manuel, alisema mnamo mwezi Januari.

Mnamo Aprili 2022, Kadinali wa Lisbon na kasisi mkuu wa Kanisa la Ureno Manuel Clemente alisema yuko tayari "kutambua makosa ya zamani" na "kuomba msamaha" kutoka kwa waathiriwa. Amehudhuria Jumatatu uwasilishaji wa ripoti ya tume huru.

'Vita kamili'

Akiwa amekabiliwa na maelfu ya visa vya unyanyasaji wa kijinsia unaofanywa na makasisi kufichuka duniani kote na shutuma za kufichwa na makasisi, Papa Francis aliahidi mwaka wa 2019 kupigana "vita vya kila namna" dhidi ya uhalifu dhidi ya watoto katikaKanisa.

Kabla ya Ureno, nchi kadhaa tayari zimejaribu kuchukua hatua ya jambo hili, ikiwa ni pamoja na Ufaransa, Ireland, Ujerumani, Australia na Uholanzi.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.