Pata taarifa kuu

Urusi kupiga marufuku uuzaji wa mafuta yake kwa nchi ambazo zinaweka kikomo cha bei

Kuanzia Februari 1, 2023, Urusi itapiga marufuku uuzaji wa mafuta yake kwa nchi za kigeni zinazotumia kikomo ch bei mafuta ya Urusi. Nchi za Magharibi, ambazo zinataka kuweka kikomo rasilimali za Moscow zilizokusudiwa kufadhili vita vya Ukraine, tayari zinashuhudia vikwazo vya mafuta ya Urusi. Hatua hiyo, iliyoamuliwa na Kremlin, itatumika hadi Julai 1, Vladimir Putin akizingatia haki ya kusamehe baadhi ya nchi.

Kiwanda cha kuzalisha dizeli katika kisima cha mafuta cha Yarakta, kinachomilikiwa na Kampuni ya Mafuta ya Irkutsk (INK), katika eneo la Irkutsk, Urusi. Umoja wa Ulaya unatayarisha awamu ya sita ya vikwazo dhidi ya Urusi ambavyo vinaweza kujumuishwa kuwekewa vikwazo vya uagizaji wa mafuta ya Urusi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, wanadiplomasia wawili wa Ulaya walisema Mei 1.
Kiwanda cha kuzalisha dizeli katika kisima cha mafuta cha Yarakta, kinachomilikiwa na Kampuni ya Mafuta ya Irkutsk (INK), katika eneo la Irkutsk, Urusi. Umoja wa Ulaya unatayarisha awamu ya sita ya vikwazo dhidi ya Urusi ambavyo vinaweza kujumuishwa kuwekewa vikwazo vya uagizaji wa mafuta ya Urusi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, wanadiplomasia wawili wa Ulaya walisema Mei 1. REUTERS - VASILY FEDOSENKO
Matangazo ya kibiashara

Kikomo cha bei ya mafuta ya Urusi - dola 60 kwa pipa - ambacho kimeamuliwa na Umoja wa Ulaya, nchi zilizostawi kiuchumi (G7) na Australia, kinahusu mafuta yanayouzwa kwa meli kwa nchi za ulimwengu wa tatu. Hatua hiyo, iliyoanza kutumika tarehe 5 Desemba, inaendana na vikwazo vya mafuta katika nchi hizo.

Hatua hii inalenga kuzuia Moscow kukwepa vikwazo kwa kuwauzia nchi zingine kiasi ambacho nchi za Magharibi hawanunui tena kutoka humo. Kwa kupiga marufuku, kuanzia Februari 1, 2023, kuwauzia wale wanaotumia kikomo cha bei , Rais wa Urusi Vladimir Putin anatarajia kuhimiza wanunuzi kutoheshimu maamuzi ya nchi za Magharibi, huku akizingatia uhusiano wake wa kibiashara na nchi zinazoonekana kuwa za kirafiki.

Lakini kwa sasa, hakuna kinachosema kuwa hatua hii italeta madhara, kwa sababu makampuni ya bima ya nchi za Magharibi sasa yanakataa kutoa huduma kwa meli za mafuta kutoka nchi ambazo zitatumia kikomo cha bei ya mafuta. Hata hivyo, kampuni za bima za nchi za Magharibi zinawakilisha 90% ya bima ya mafuta ya baharini. Haiwezekani kufanya hivyo bila kampuni hizo. Hata Uturuki imedokeza kuwa meli za mafuta zisizo na bima hazitaweza tena kutumia njia zake.

Kulingana na shirika la Bloomberg, mauzo ya mafuta tayari yamepungua kwa 54% katika wiki baada ya kutekelezwa kwa maamuzi ya nchi za Magharibi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.