Pata taarifa kuu

Tume ya Ulaya yapendekeza kuzuia zaidi ya euro bilioni 13 zinazopelekwa Hungary

Tume ya Umoja wa Ulaya inaona kuwa hatua zilizowekwa na serikali ya Hungary katika suala la haki na vita dhidi ya ufisadi hazitoshi. Nchi Wanachama zina hadi Desemba 19 kupiga kura kwa wingi ili kutoa uamuzi wao.

Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban anahudhuria mjadala ulioandaliwa na mashirika ya uchapishaji kuhusu 'Dhoruba juu ya Ulaya - vita vya Ukraine, mgogoro wa nishati na changamoto za kijiografia na kisiasa' huko Berlin, Ujerumani, Jumanne, Oktoba 11, 2022.
Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban anahudhuria mjadala ulioandaliwa na mashirika ya uchapishaji kuhusu 'Dhoruba juu ya Ulaya - vita vya Ukraine, mgogoro wa nishati na changamoto za kijiografia na kisiasa' huko Berlin, Ujerumani, Jumanne, Oktoba 11, 2022. AP - Markus Schreiber
Matangazo ya kibiashara

Tume ya Ulaya imependekeza, Jumatano, Novemba 30, kuzuia euro bilioni 7.5 za fedha za uwiano na bilioni 5.8 za mpango wa wa uzinduzi uliokusudiwa kwa Hungary. Taasisi hiyo imetoa wito wa kutoa fedha hizi pindi tu haki na mageuzi ya kupambana na ufisadi yatatekelezwa ipasavyo.

Utaratibu wa "masharti", unaokusudiwa kulinda bajeti ya Ulaya dhidi ya uvunjaji wa sheria, ulizinduliwa dhidi ya Hungariy mwezi Aprili. Uamuzi huu, wa kwanza kwa EU, ulichukuliwa hasa kutokana na "ukiukwaji wa utaratibu katika utoaji wa mikataba ya umma", pamoja na "kushindwa" katika suala la kesi za kisheria na mapambano dhidi ya rushwa.

Marekebisho yasiyotosha

Matarajio ya kunyimwa pesa yalisababisha Budapest kuanzisha hatua 17 za kujibu wasiwasi wa Brussels. Tume ya Ulaya kwa mfano imeunda "chombo huru" kwa minajili ya kudhibiti vyema matumizi ya fedha za EU, zinazoshukiwa kuwatajirisha ndugu na washirika wa karibu wa Viktor Orban. Hata hivyo, Tume inaona kuwa mageuzi haya hayakufanywa kwa njia ya sahihi hadi kufikia tarehe ya mwisho Novemba 19. Afisa mkuu wa Umojha wa Ulaya aliweka makataa haya mnamo mwez Septemba ili kuipa Hungary nafasi ya kuepuka kuzuiwa kwa euro bilioni 7.5 (karibu 20% ya fedha za Ulaya ambazo ingelipata kwa miaka ya 2021 hadi 2027).

Tume ya Ulaya pia imeamua kuhalalisha mpango wa uokoaji wa baada ya Uviko-19 (euro bilioni 5.8) lakini kwa kuambatanisha masharti 27, ambayo ni pamoja na hatua 17 za kupambana na ufisadi, pamoja na mageuzi ya kuboresha uhuru wa mahakama. "Hakuna utoaji wa fedha utakaofanyika hadi masharti haya muhimu yatimizwe ipasavyo," Naibu Mkuu wa tume hiyo, Valdis Dombrovskis, amesema siku ya Jumatano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.