Pata taarifa kuu

Ureno: Mtandao wa wasafirishaji wa wafanyakazi wahamiaji wavunjwa

Nchini Ureno, operesheni kwenye mashamba kusini mwa nchi hiyo umesambaratisha mtandao wa wasafirishaji haramu wa wafanyakazi wahamiaji, wanaoishi katika mazingira yanayochukuliwa kama utumwa. Watu thelathini na watano wamekamatwa.

Maafisa wa polisi 400 na askari wamehamasishwa kuingilia kati huko Alentejo, katikati mwa Ureno, ambako kuna mashamba makubwa yanayohitaji vibarua.
Maafisa wa polisi 400 na askari wamehamasishwa kuingilia kati huko Alentejo, katikati mwa Ureno, ambako kuna mashamba makubwa yanayohitaji vibarua. © RFI-Marie-Line Darcy
Matangazo ya kibiashara

Operesheni hiyo iliandaliwa kwa uangalifu tangu mwezi Januari mwaka huu: maafisa wa polisi 400 na askari wamehamasishwa kuingilia kati huko Alentejo, katikati mwa Ureno, ambapo kuna mashamba makubwa yanayohitaji nguvu kazi. Mtandao haramu  wa walanguzi umesambaratishwa.

Ukiongozwa na Waromania kadhaa, mtandao huo unajumuisha Wareno kadhaa wanaohudumu kama wapatanishi katika mashamba ili kuajiri wahamiaji walioajiriwa na kuwa chini ya ushawishi wao. Wahamiaji hao walikuwa wanaishi katika nusu utumwa baada ya vyeti vyao kuchukuliwa, mishahara kupunguzwa hadi euro 5 au 10 kwa siku, huku wakikabiliwa na unyanyasaji wa kisaikolojia na kimwili hali ambayo imekuwa ikiwalazimu wahamiaji hao kuishi katika hali ya utumwa usio wa kawaida.

Angalau wafanyakazi 200 kutoka nchi tofauti kama Nepal, India, Moldova, Timor Mashariki au Morocco, waathiriwa wa mtandao, hivyo ndivyo walivyogunduliwa. Hali ya maisha yao ilikuwa ya kusikitisha kabisa. Wahamiaji hawa, kwa sehemu kubwa, wanataka kuendelea kufanya kazi kwenye mashamba. Lakini kipindi cha baridi kinaingia na mikataba ya ajira imesitishwa. Kipaumbele cha mamlaka na vyama vya kujisaidia sasa ni kuwa na uwezo wa kuwapatishia upya makazi wafanyakazi hawa kwa heshima.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.