Pata taarifa kuu

Mfumuko wa bei: Ureno yatangaza msaada wa euro bilioni 2.4 kwa raia wake

Serikali ya Ureno imetangaza kifurushi cha hatua za kusaidia kaya kukabiliana na mfumuko wa bei cha euro bilioni 2.4, ambacho kitajumuisha kupunguzwa kwa ushuru wa nishati.

Waziri Mkuu wa Ureno Antonio Costa akitoa hotuba Januari 30, 2022 baada ya ushindi wake katika uchaguzi wa mapema wa wabunge.
Waziri Mkuu wa Ureno Antonio Costa akitoa hotuba Januari 30, 2022 baada ya ushindi wake katika uchaguzi wa mapema wa wabunge. Getty Images - Horacio Villalobos
Matangazo ya kibiashara

Msaada sawa na takriban 1% ya Pato la Taifa. Serikali ya Ureno ilizindua Jumatatu, Septemba 5, kifurushi cha hatua za kusaidia kaya kukabiliana na mfumuko wa bei, hadi euro bilioni 2.4, ambacho kitajumuisha kupunguzwa kwa ushuru wa nishati. Mpango huu wa hatua nane unaoitwa "familia kwanza" unakuja pamoja na msaada wa bilioni 1.6 ambao tayari umetolewa hadi Septemba.

"Ni miaka thelathini tangu tumeona ongezeko kubwa na la ghafla la gharama ya maisha," alisema Waziri Mkuu Antonio Costa, huku akitetea "tahadhari nyingi ili kukabiliana na mfumko wa bei" . Kwa hivyo serikali inapanga kulipa hundi ya euro 125 kwa kila mtu, iliyoongezeka kwa euro 50 kwa kila mtoto, kwa Mreno anayepata hadi euro 2,700 kila mwezi.

Kuongezeka kwa mafao ya pensheni za kustaafu

Serikali ya kisoshalisti pia imetoa msaada wa moja kwa moja kwa familia na ongezeko la kipekee la mafao ya pensheni za kustaafu, Waziri Mkuu alisema katika mkutano na waandishi wa habari. Kwa hivyo, wastaafu watapata nyongeza sawa na nusu ya pensheni yao ya kila mwezi.

Nchini Ureno, bei za watumiaji ziliongezeka mwezi Agosti kwa 9% mwaka hadi mwaka, kulingana na makadirio ya muda ya Taasisi ya Kitaifa ya Takwimu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.