Iran : Putin afanya ziara nchini Tehran
Rais wa Urusi, Vladimir Putin, anafanya ziara nchini Tehran, ikiwa ziara ya pili kwake tangu taifa lake lianze uvamizi nchini Ukraine.
Imechapishwa:
Putin anatarajiwa kukutana na kiongozi wa Tehran, Ayatollah Ali Khamenei, na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.
Baadhi ya maswala yanayotarajiwa kujadiliwa na viongozi hao watatu ni pamoja na uzaji wa ngano, hali nchini Ukraine na Syria.
Tangu kuanza kwa vita nchini Ukrain, rais Putin, amekuwa kifanya ziara kwa mataifa yaliokuwa chini ya muungano wa Soviet, mwezi uliopita akizuru mataifa ya Tajikistan naTurkmenistan.
Ziara ya Putin nchini Tehran inatoa nafasi kwake kuimarisha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili, ambayo yote yamewekewa vikwazo vya kiuchumi na wenzao wa magharibi.
Ziara hii pia inajiri kipindi hiki, Tehran ikituhumiwa na Marekani kwa kuwa na njama kuipa Urusi ndege za kivita ambazo hazina rubani kutumika kwa vita vinavyoendelea nchini Ukraine.